1Nahashi yule Mwamoni, akakwea kuuzunguka kwa jeshi mji wa Yabeshi-Gileadi. Watu wote wa Yabeshi wakamwambia, âFanya mkataba na sisi, na tutakuwa chini yako.â
2Lakini Nahashi yule Mwamoni akajibu, âNitafanya mkataba na ninyi tu kwa sharti kwamba nitangĘźoa jicho la kulia la kila mmoja wenu, na hivyo kuleta aibu juu ya Israeli yote.â
3Viongozi wa Yabeshi wakamwambia, âTupe siku saba ili tuweze kutuma wajumbe katika Israeli yote, kama hakuna hata mmoja anayekuja kutuokoa, tutajisalimisha kwako.â
4Wajumbe walipofika Gibea ya Sauli na kutoa taarifa juu ya masharti haya kwa watu, wote walilia kwa sauti kubwa.
5Wakati huo huo Sauli alikuwa anarudi kutoka mashambani, akiwa nyuma ya maksai wake, naye akauliza, âWatu wana nini? Mbona wanalia?â Ndipo wakamweleza jinsi watu wa Yabeshi walivyokuwa wamesema.
6Sauli aliposikia maneno yao, Roho wa Mungu akaja juu yake kwa nguvu, naye akawaka hasira.
7Akachukua jozi ya maksai na kuwakata vipande vipande, naye kuvituma hivyo vipande kupitia wajumbe katika Israeli yote, wakitangaza, âHivi ndivyo itakavyofanyika kwa maksai wa kila mmoja ambaye hatamfuata Sauli na Samweli.â Kisha hofu ya Bwana ikawaangukia watu, nao wakatoka kama mtu mmoja.
8Sauli alipowakusanya huko Bezeki, watu wa Israeli walikuwa 300,000 na watu wa Yuda 30,000.
9Wakawaambia wale wajumbe waliokuwa wamekuja, âWaambieni watu wa Yabeshi-Gileadi, âKesho kabla jua halijawa kali, mtaokolewa.â â Wajumbe walipokwenda na kutoa taarifa hii kwa watu wa Yabeshi, wakafurahi.
10Wakawaambia Waamoni, âKesho tutajisalimisha kwenu, nanyi mtaweza kututendea chochote mnachoona chema kwenu.â
11Kesho yake Sauli alitenganisha watu wake katika vikosi vitatu; wakati wa zamu ya mwisho ya usiku wakaingia katika kambi ya Waamoni na kuwachinja mpaka mchana. Wale walionusurika wakasambaa, kiasi kwamba hawakusalia watu wawili pamoja.
12Kisha watu wakamwambia Samweli, âNi nani yule aliyeuliza, âJe, Sauli atatawala juu yetu?â Tuletee hawa watu, nasi tutawaua.â
13Lakini Sauli akasema, âHakuna hata mmoja atakayeuawa leo, kwa kuwa siku hii Bwana ameokoa Israeli.â
14Ndipo Samweli akawaambia watu, âNjooni, twendeni Gilgali na huko tuthibitishe ufalme.â
15Kwa hiyo watu wote wakaenda Gilgali na kumthibitisha Sauli kuwa mfalme mbele za Bwana. Huko wakatoa dhabihu za sadaka za amani mbele za Bwana, naye Sauli na Waisraeli wote wakafanya karamu kubwa.