Inapakia...
📖

Biblia Takatifu

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™
BIB 17 mistari

Wimbo Ulio Bora 1

Wimbo Ulio Bora • Sura 1 / 8

1Wimbo ulio bora wa Solomoni.

Shairi La Kwanza

2Unibusu kwa busu la kinywa chako,kwa maana upendo wako unafurahisha kuliko divai.

3Manukato yako yananukia vizuri,jina lako ni kama manukato yaliyomiminwa.Ndiyo sababu wanawali wanakupenda!

4Nichukue twende nawe, na tufanye haraka!
Mfalme na anilete ndani ya vyumba vyake.MarafikiTunakushangilia na kukufurahia,
tutasifu upendo wako zaidi kuliko divai.MpendwaTazama jinsi ilivyo bora wakupende!

5Mimi ni mweusi, lakini napendeza,enyi binti za Yerusalemu,
mweusi kama mahema ya Kedari,
kama mapazia ya hema la Solomoni.

6Usinikazie macho kwa sababu mimi ni mweusi,kwa sababu nimefanywa mweusi na jua.Wana wa mama yangu walinikasirikiana kunifanya niwe mtunza mashamba ya mizabibu.
Shamba langu mwenyewe la mizabibu nimeliacha.

7Niambie, wewe ambaye ninakupenda,unalisha wapi kundi lako la kondoo
na ni wapi unapowapumzisha kondoo wako adhuhuri.Kwa nini niwe kama mwanamke aliyefunikwa shelakaribu na makundi ya rafiki zako?

8Kama hujui, ewe mwanamke mzuri kuliko wote,fuata nyayo za kondoo,na kulisha wana-mbuzi wakokaribu na hema za wachungaji.

9Mpenzi wangu, ninakufananisha na farasi jikealiyefungwa katika mojawapo ya magari ya vita ya Farao.

10Mashavu yako yanapendeza yakiwa na vipuli,shingo yako ikiwa na mikufu ya vito.

11Tutakufanyia vipuli vya dhahabu,vyenye kupambwa kwa fedha.

12Wakati mfalme alipokuwa mezani pake,manukato yangu yalisambaza harufu yake nzuri.

13Mpenzi wangu kwangu mimi ni kifuko cha manemanekati ya matiti yangu.

14Mpenzi wangu kwangu mimi ni kama kishada cha maua ya mhinakutoka mashamba ya mizabibu ya En-Gedi.

15Tazama jinsi ulivyo mzuri, mpenzi wangu!Tazama jinsi ulivyo mzuri!
Macho yako ni kama ya hua.

16Tazama jinsi ulivyo mzuri, mpenzi wangu!Ee, tazama jinsi unavyopendeza!
Na kitanda chetu ni cha majani mazuri.

17Nguzo za nyumba yetu ni mierezi,na mapao yetu ni miberoshi.