1Maono ya Obadia.
Hili ndilo asemalo Bwana Mwenyezi kuhusu Edomu:Tumesikia ujumbe kutoka kwa Bwana:Mjumbe alitumwa kwa mataifa kusema,“Inukeni, twendeni tukapigane vita dhidi yake.”
2“Angalieni, nitawafanya wadogo miongoni mwa mataifa,mtadharauliwa kabisa.
3Kiburi cha moyo wako kimekudanganya,wewe unayeishi katika majabali ya miamba
na kufanya makao yako juu,wewe unayejiambia mwenyewe,‘Ni nani awezaye kunishusha chini?’
4Ingawa unapaa juu kama taina kufanya kiota chako kati ya nyota,
nitakushusha chini kutoka huko,”asema Bwana.
5“Ikiwa wevi wangekuja kwako,ikiwa wanyangʼanyi wangekujia usiku:Lo! Tazama ni maafa kiasi gani yangekuwa yanakungojea:je, si wangeiba tu kiasi ambacho wangehitaji?Kama wachuma zabibu wangekuja kwako,je, wasingebakiza zabibu chache?
6Lakini tazama jinsi Esau atakavyotekwa,jinsi hazina zake zilizofichwa zitatekwa nyara!
7Wote ulioungana nao watakufukuza hadi mpakani,rafiki zako watakudanganya na kukushinda,wale wanaokula mkate wako watakutegea mtego,lakini hutaweza kuugundua.
8“Katika siku hiyo,” asema Bwana,“je, sitaangamiza watu wenye hekima wa Edomu,
watu wenye ufahamu katika milima ya Esau?
9Ee Temani, mashujaa wako watatiwa hofu,kila mmoja katika milima ya Esau
ataangushwa chini kwa kuchinjwa.
10Kwa sababu ya jeuri uliyofanya dhidi ya ndugu yako Yakobo,aibu itakufunika;
utaangamizwa milele.
11Siku ile ulisimama mbali ukiangaliawakati wageni walipojichukulia utajiri wakena watu wa nchi nyingine walipoingia malango yakewakipiga kura kwa ajili ya Yerusalemu,
ulikuwa kama mmoja wao.
12Usingemdharau ndugu yakokatika siku ya msiba wake,wala kufurahia juu ya watu wa Yudakatika siku ya maangamizi yao,wala kujigamba sanakatika siku ya taabu yao.
13Usingeingia katika malango ya watu wangukatika siku ya maafa yao,wala kuwadharau katika janga laokatika siku ya maafa yao,wala kunyangʼanya mali zaokatika siku ya maafa yao.
14Usingengoja kwenye njia pandana kuwaua wakimbizi wao,wala kuwatoa watu wake waliosaliakatika siku ya shida yao.
15“Siku ya Bwana iko karibukwa mataifa yote.Kama ulivyofanya, nawe utafanyiwa vivyo hivyo,matendo yako yatakurudia juu ya kichwa chako.
16Kama vile ulivyokunywa juu ya mlima wangu mtakatifu,vivyo hivyo mataifa yote watakunywa mfululizo,watakunywa na kunywa,nao watatoweka kana kwamba hawajawahi kuwepo.
17Lakini katika Mlima Sayuni kutakuwepona wale watakaookoka;
nao utakuwa mtakatifu,nayo nyumba ya Yakoboitamiliki urithi wake.
18Nyumba ya Yakobo itakuwa moto,na nyumba ya Yosefu itakuwa mwali wa moto;nayo nyumba ya Esau itakuwa bua kavu,nao wataiwasha moto na kuiteketeza.Hakutakuwa na watakaosalimikakutoka nyumba ya Esau.”Bwana amesema.
19Watu kutoka nchi ya Negebuwataikalia milima ya Esau,na watu kutoka miteremko ya vilimawatamiliki nchi ya Wafilisti.Watayakalia mashamba ya Efraimu na Samaria,naye Benyamini atamiliki Gileadi.
20Kundi la Waisraeli walioko uhamishoni Kanaaniwatarudi na kumiliki nchi mpaka Sarepta.Walioko uhamishoni Sefaradi kutoka Yerusalemuwatamiliki miji ya Negebu.
21Waokoaji watakwea juu ya Mlima Sayunikutawala milima ya Esau.
Nao ufalme utakuwa wa Bwana.