1Ujumbe: Neno la Bwana kwa Israeli kupitia kwa Malaki.
2Bwana asema, âNimewapenda ninyi.â âLakini ninyi mnauliza, âWewe umetupendaje?â â Bwana asema, âJe, Esau hakuwa ndugu yake Yakobo? Hata hivyo nimempenda Yakobo,
3lakini nikamchukia Esau, nami nimeifanya milima yake kuwa ukiwa, na urithi wake nimewapa mbweha wa jangwani.â
4Edomu anaweza kusema, âIngawa tumepondapondwa, tutajenga upya magofu.â Lakini hili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote asemalo: âWanaweza kujenga, lakini nitabomoa. Wataitwa Nchi Ovu, watu ambao siku zote wapo chini ya ghadhabu ya Bwana.
5Mtayaona kwa macho yenu wenyewe na kusema, âBwana ni mkuu, hata nje ya mipaka ya Israeli!â
6âMwana humheshimu baba yake, naye mtumishi humheshimu bwana wake. Kama mimi ni baba, iko wapi heshima ninayostahili? Kama mimi ni bwana, iko wapi heshima ninayostahili?â asema Bwana Mwenye Nguvu Zote. âNi ninyi, enyi makuhani, mnaolidharau Jina langu. âLakini mnauliza, âTumelidharau Jina lako kwa namna gani?â
7âMnatoa sadaka chakula kilichotiwa unajisi juu ya madhabahu yangu. âLakini ninyi mnauliza, âTumekutia unajisi kwa namna gani?â âKwa kusema kuwa meza ya Bwana ni ya kudharauliwa.
8Wakati mletapo dhabihu za wanyama walio vipofu, je, hilo si kosa? Mnapoleta dhabihu zilizo vilema au wanyama wagonjwa, je, hilo si kosa? Jaribuni kuvitoa kwa mtawala wenu! Je, angefurahishwa nanyi? Je, atawakubalia?â asema Bwana Mwenye Nguvu Zote.
9âBasi mwombeni Mungu awe na neema kwetu. Je, kwa sadaka kama hizo kutoka mikononi mwenu, atawapokea?â asema Bwana Mwenye Nguvu Zote.
10âLaiti mmoja wenu angalifunga milango ya Hekalu, ili msije mkawasha moto usiokuwa na faida juu ya madhabahu yangu! Sina furaha nanyi,â asema Bwana Mwenye Nguvu Zote, ânami sitaikubali sadaka toka mikononi mwenu.
11Jina langu litakuwa kuu miongoni mwa mataifa, kuanzia mawio ya jua hata machweo yake. Kila mahali uvumba na sadaka safi zitaletwa kwa Jina langu, kwa sababu Jina langu litakuwa kuu miongoni mwa mataifa,â asema Bwana Mwenye Nguvu Zote.
12âLakini mnalinajisi Jina langu kwa kusema kuhusu meza ya Bwana, âImetiwa unajisi pamoja na chakula chake. Ni ya kudharauliwa.â
13Nanyi mnasema, âMzigo gani huu!â Nanyi mnaidharau kwa kiburi,â asema Bwana Mwenye Nguvu Zote. âWakati mnapowaleta wanyama mliopokonya kwa nguvu, walio vilema au walio wagonjwa na kuwatoa kama dhabihu, je, niwakubali kutoka mikononi mwenu?â asema Bwana.
14âAmelaaniwa yeye adanganyaye, aliye na mnyama wa kiume anayekubalika katika kundi lake na kuweka nadhiri ya kumtoa, lakini akatoa dhabihu ya mnyama aliye na dosari kwa Bwana. Kwa kuwa mimi ni Mfalme Mkuu, nalo Jina langu linapaswa kuogopwa miongoni mwa mataifa,â asema Bwana Mwenye Nguvu Zote.