1Neno la Bwana ambalo lilimjia Yoeli mwana wa Pethueli.
2Sikilizeni hili, enyi wazee;sikilizeni, ninyi nyote mnaoishi katika nchi.Je, jambo kama hili lilishawahi kutokeakatika siku zenu au katika siku za babu zenu?
3Waelezeni watoto wenu,na watoto wenu wawaambie watoto wao,
na watoto wao kwa kizazi kitakachofuata.
4Kilichosazwa na kundi la tunutunzige wakubwa wamekula,kilichosazwa na nzige wakubwaparare wamekula,kilichosazwa na pararemadumadu wamekula.
5Amkeni, enyi walevi, mlie!Pigeni yowe enyi wanywaji wote wa mvinyo,pigeni yowe kwa sababu ya mvinyo mpya,kwa kuwa mmenyangʼanywa
kutoka midomoni mwenu.
6Taifa limevamia nchi yangu,lenye nguvu tena lisilo na idadi;lina meno ya simba,magego ya simba jike.
7Limeharibu mizabibu yanguna kuangamiza mitini yangu.Limebambua magome yakena kuyatupilia mbali,
likayaacha matawi yake yakiwa meupe.
8Omboleza kama bikira aliyevaa nguo ya guniaanayehuzunika kwa ajili ya mume wa ujana wake.
9Sadaka za nafaka na sadaka za kinywajizimekatiliwa mbali kutoka nyumba ya Bwana.Makuhani wanaomboleza,wale wanaohudumu mbele za Bwana.
10Mashamba yameharibiwa,ardhi imekauka;nafaka imeharibiwa,mvinyo mpya umekauka,
mafuta yamekoma.
11Kateni tamaa, enyi wakulima,lieni, enyi mlimao mizabibu;huzunikeni kwa ajili ya ngano na shayiri,kwa sababu mavuno ya shambani yameharibiwa.
12Mzabibu umekaukana mtini umenyauka;mkomamanga, mtende na mtofaa,miti yote shambani, imekauka.Hakika furaha yote ya mwanadamuimeondoka.
13Vaeni nguo ya gunia, enyi makuhani, muomboleze;pigeni yowe, enyi mnaohudumu madhabahuni.Njooni, vaeni nguo ya gunia usiku kucha,enyi mnaohudumu mbele za Mungu wangu;kwa kuwa sadaka za nafaka na sadaka za kinywajizimezuiliwa kufika katika nyumba ya Mungu wenu.
14Tangazeni saumu takatifu;liiteni kusanyiko takatifu.Iteni wazeena wote waishio katika nchiwaende katika nyumba ya Bwana Mungu wenu,wakamlilie Bwana.
15Ole kwa siku hiyo!Kwa kuwa siku ya Bwana iko karibu;itakuja kama uharibifukutoka kwa Mwenyezi.*
16Je, chakula hakikukatiliwa mbalimbele ya macho yetu:furaha na shangwekutoka nyumba ya Mungu wetu?
17Mbegu zinakaukachini ya mabonge ya udongo.Ghala zimeachwa katika uharibifu,ghala za nafaka zimebomolewa,
kwa maana hakuna nafaka.
18Jinsi gani ngʼombe wanavyolia!Makundi ya mifugo yanahangaikakwa sababu hawana malisho;hata makundi ya kondoo yanateseka.
19Kwako, Ee Bwana, naita,kwa kuwa moto umeteketeza
malisho ya mbuganina miali ya moto imeunguzamiti yote shambani.
20Hata wanyama wa porini wanakuonea shauku;vijito vya maji vimekauka,na moto umeteketezamalisho yote ya mbugani.
Tanbihi
Mwenyezi hapa ina maana ya Shaddai kwa Kiebrania.