Inapakia...
📖

Biblia Takatifu

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™
BIB 16 mistari

Mika 1

Mika • Sura 1 / 7

1Neno la Bwana lilimjia Mika, Mmoreshethi, wakati wa utawala wa Yothamu, Ahazi na Hezekia, wafalme wa Yuda; ufunuo aliouona kuhusu Samaria na Yerusalemu.

2Sikieni, enyi mataifa, enyi nyote,sikilizeni, ee dunia na wote mliomo ndani yake,ili Bwana Mwenyezi ashuhudie dhidi yenu,Bwana kutoka Hekalu lake takatifu.

Hukumu Dhidi Ya Samaria Na Yerusalemu

3Tazama! Bwana anakuja kutoka mahali pake;anashuka na kukanyaga
mahali palipoinuka juu pa dunia.

4Milima inayeyuka chini yakena mabonde yanagawanyikakama nta mbele ya moto,kama maji yatiririkayo kasi
kwenye mteremko.

5Yote haya ni kwa sababu ya kosa la Yakobo,ni kwa sababu ya dhambi za nyumba ya Israeli.Kosa la Yakobo ni lipi?Je, sio Samaria?Je, mahali pa juu pa Yuda pa kuabudia miungu ni nini?Je, sio Yerusalemu?

6“Kwa hiyo nitaufanya Samaria kuwa lundo la kokoto,mahali pa kuotesha mizabibu.Nitayamwaga mawe yake katika bondena kuacha wazi misingi yake.

7Sanamu zake zotezitavunjwa vipande vipande;zawadi zake zote za Hekaluzitachomwa kwa moto;
nitaharibu vinyago vyake vyote.Kwa kuwa alikusanya zawadi zakekutokana na ujira wa kahaba,nazo zitatumika tenakulipa mishahara ya kahaba.”

Kulia Na Kuomboleza

8Kwa ajili ya hili nitalia na kuomboleza;nitatembea bila viatu na tena uchi.Nitabweka kama mbwehana kuomboleza kama bundi.

9Kwa sababu jeraha lake halitibiki;limekuja Yuda.Limefika hasa kwenye lango la watu wangu,hata Yerusalemu kwenyewe.

10Usiliseme hili huko Gathi;usilie hata kidogo.Huko Beth-le-Afragaagaa mavumbini.

11Piteni mkiwa uchi na wenye aibu,ninyi mkaao Shafiri.Wale waishio Saananihawatatoka nje.Beth-Eseli iko katika maombolezo;kinga yake imeondolewa kwako.

12Wale waishio Marothi wanagaagaa kwa maumivuwakingoja msaada,kwa sababu maangamizi yamekujakutoka kwa Bwana,
hata katika lango la Yerusalemu.

13Enyi mkaao Lakishi,fungeni farasi kwenye magari ya vita.Mlikuwa chanzo cha dhambikwa Binti Sayuni,kwa kuwa makosa ya Israeliyalikutwa kwako.

14Kwa hiyo utaipa Moresheth-Gathizawadi za kuagana.Mji wa Akzibu utaonyesha wazi udanganyifukwa wafalme wa Israeli.

15Nitawaleteeni atakayewashindaninyi mnaoishi Maresha.Yeye aliye utukufu wa Israeliatakuja Adulamu.

16Nyoeni nywele zenu katika kuombolezakwa ajili ya watoto wenu mnaowafurahia;jifanyieni upara kama tai,kwa kuwa watawaacha
na kwenda uhamishoni.