Inapakia...
📖

Biblia Takatifu

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™
BIB 18 mistari

Sefania 1

Sefania • Sura 1 / 3

1Neno la Bwana lililomjia Sefania mwana wa Kushi, mwana wa Gedalia, mwana wa Amaria, mwana wa Hezekia, wakati wa utawala wa Yosia mwana wa Amoni mfalme wa Yuda:

Onyo La Maangamizi Yanayokuja

2Bwana asema,“Nitafagia kila kitu
kutoka kwenye uso wa dunia.”

3“Nitafagilia mbali watu na wanyama;nitafagilia mbali ndege wa angani
na samaki wa baharini.Wafanyao maovu watapata tu kokoto,nami nitamkatilia mbali mwanadamu atoke katika dunia,”asema Bwana.

Dhidi Ya Yuda

4“Nitaiadhibu Yudana wote wakaao Yerusalemu.Kutoka mahali hapa nitakatilia mbalikila mabaki ya Baali,majina ya wapagani na makuhaniwaabuduo sanamu:

5wale ambao husujudu juu ya mapaakuabudu jeshi la vitu vya angani,wale ambao husujudu na kuapa kwa Bwanana ambao pia huapa kwa Malkamu,

6wale wanaoacha kumfuata Bwana,wala hawamtafuti Bwana
wala kutaka shauri lake.

7Nyamazeni mbele za Bwana Mwenyezi,kwa maana siku ya Bwana iko karibu.Bwana ameandaa dhabihu,amewaweka wakfu wale aliowaalika.

8Katika siku ya dhabihu ya Bwananitawaadhibu wakuu
na wana wa mfalmena wale wote wanaovaanguo za kigeni.

9Katika siku hiyo nitaadhibu wote ambaohukwepa kukanyaga kizingiti,ambao hujaza hekalu la miungu yaokwa dhuluma na udanganyifu.”

10Bwana asema, “Katika siku hiyokilio kitapanda juu kutoka lango la Samaki,
maombolezo kutoka mtaa wa pili,
na mshindo mkubwa kutoka vilimani.

11Ombolezeni, ninyi mnaoishi katika eneo la sokoni;wafanyabiashara wenu wote wameangamizwa,wote ambao wanafanya biashara ya fedhawataangamizwa.

12Wakati huo nitasaka mji wa Yerusalemu kwa taa,na kuwaadhibu wale ambao
wanakaa katika hali ya kuridhika,ambao ni kama divaiiliyobaki kwenye machicha,ambao hudhani, ‘Bwana hatafanya lolote,jema au baya.’

13Utajiri wao utatekwa nyara,nyumba zao zitabomolewa.Watajenga nyumba,lakini hawataishi ndani yake;watapanda mizabibulakini hawatakunywa divai yake.

Siku Kubwa Ya Bwana

14“Siku kubwa ya Bwana iko karibu:iko karibu na inakuja haraka.Sikilizeni! Kilio katika siku ya Bwanakitakuwa kichungu,
hata shujaa atapiga kelele.

15Siku ile ni siku ya ghadhabu,siku ya fadhaa na dhiki,siku ya uharibifu na ukiwa,siku ya giza na utusitusi,
siku ya mawingu na giza nene,

16siku ya tarumbeta na mlio wa vitadhidi ya miji yenye ngome
na dhidi ya minara mirefu.

17Nitawaletea watu dhiki,nao watatembea kama vipofu,kwa sababu wametenda dhambidhidi ya Bwana.Damu yao itamwagwa kama vumbina matumbo yao kama taka.

18Fedha yao wala dhahabu yaohazitaweza kuwaokoa
katika siku hiyo ya ghadhabu ya Bwana.Katika moto wa wivu wakedunia yote itateketezwa,kwa maana ataleta mwishowa wote wanaoishi katika dunia ghafula.”