Inapakia...
📖

Biblia Takatifu

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™
BIB 27 mistari

Amosi 5

Amosi • Sura 5 / 9

Maombolezo Na Wito Wa Toba

1Sikia neno hili, ee nyumba ya Israeli, ombolezo hili ninalifanya kuwahusu ninyi:

2“Bikira Israeli ameanguka,kamwe hatainuka tena,ameachwa pweke katika nchi yake,hakuna yeyote wa kumwinua.”

3Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo:“Wakati mmoja wa miji yako utakapopeleka watu elfu moja vitani kwa ajili ya Israeli,mia moja tu watarudi;wakati mji utakapopeleka mia moja,kumi tu ndio watarudi hai.”

4Hili ndilo Bwana asemalo kwa nyumba ya Israeli:“Nitafuteni mpate kuishi;

5msitafute Betheli,msiende Gilgali,msisafiri kwenda Beer-Sheba.Kwa maana kwa hakika Gilgali itakwenda uhamishoni,na Betheli itafanywa kuwa si kitu.”*

6Mtafuteni Bwana mpate kuishi,au atafagia nyumba ya Yosefu kama moto;utawateketeza, nayo Bethelihaitakuwa na yeyote wa kuuzima.

7Ninyi ambao mnageuza haki kuwa uchunguna kuiangusha haki chini

8(yeye ambaye alifanya Kilimia na Orioni,ambaye hugeuza giza kuwa mapambazuko
na mchana kuwa usiku,ambaye huyaita maji ya baharina kuyamwaga juu ya uso wa nchi:
Bwana ndilo jina lake;

9yeye hufanya maangamizo kwenye ngomena kufanya mji uliozungushiwa ngome kuwa ukiwa),

10mnamchukia yule akemeaye mahakamani,na kumdharau yule ambaye husema kweli.

11Mnamgandamiza maskinina kumlazimisha awape nafaka.Kwa hiyo, ingawa mmejenga majumba ya mawe ya fahari,hamtaishi ndani yake;ingawa mmepanda mashamba mazuri ya mizabibu,hamtakunywa divai yake.

12Kwa kuwa ninajua hesabu ya makosa yenuna ukubwa wa dhambi zenu.
Mmewaonea wenye haki na kupokea rushwana kuzuia haki ya maskini mahakamani.

13Kwa hiyo mtu mwenye busara hunyamaza kimya nyakati kama hizo,kwa kuwa nyakati ni mbaya.

14Tafuteni mema, wala si mabaya,ili mpate kuishi.Ndipo Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote atakuwa pamoja nanyi,kama msemavyo yupo nanyi.

15Yachukieni maovu, yapendeni mema;dumisheni haki mahakamani.Yamkini Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zoteatawahurumia mabaki ya Yosefu.

16Kwa hiyo hili ndilo Bwana, Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote, asemalo:“Kutakuwepo maombolezo katika barabara zotena vilio vya uchungu katika njia kuu zote.Wakulima wataitwa kuja kulia,na waombolezaji waje kuomboleza.

17Kutakuwepo kuomboleza katika mashamba yote ya mizabibu,kwa kuwa nitapita katikati yenu,”asema Bwana.

Siku Ya Bwana

18Ole wenu ninyi mnaoitamanisiku ya Bwana!Kwa nini mnaitamani siku ya Bwana?Siku hiyo itakuwa giza, si nuru.

19Itakuwa kama vile mtu aliyemkimbia simbakumbe akakutana na dubu,kama vile mtu aliyeingia nyumbani mwakena kuupumzisha mkono wake kwenye ukuta,
kumbe akaumwa na nyoka.

20Je, siku ya Bwana haitakuwa giza, na si nuru:giza nene, bila mwonzi wa mwanga?

21“Ninachukia, ninazidharau sikukuu zenu za dini;siwezi kuvumilia makusanyiko yenu.

22Hata ingawa mnaniletea sadaka zenu za kuteketezwa na sadaka za nafaka,sitazikubali.Ingawa mnaniletea sadaka nzuri za amani,sitazitambua.

23Niondoleeni kelele za nyimbo zenu!Sitasikiliza sauti za vinubi vyenu.

24Lakini acheni haki itiririke kama mto,na uadilifu uwe kama kijito kisichokauka!

25“Je, mliniletea dhabihu na sadakakwa miaka arobaini kule jangwani,
ee nyumba ya Israeli?

26Mmeyainua madhabahu ya mfalme wenu,Sikuthi mungu wenu mtawala,na Kiuni mungu wenu wa nyota,ambao mliwatengeneza wenyewe.

27Kwa sababu hiyo nitawapeleka uhamishoni mbali kupita Dameski,”asema Bwana, ambaye jina lake ni Mungu Mwenye Nguvu Zote.

Tanbihi

*

Yaani Aveni kwa Kiebrania, kumaanisha Beth-Aveni, jina lingine la Betheli kwa dhihaka.