Inapakia...
📖

Biblia Takatifu

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™
BIB • 16 mistari

Mhubiri 4

Mhubiri • Sura 4 / 12

Uonevu, Taabu, Uadui

1Nikatazama tena nikaona uonevu wote uliokuwa unafanyika chini ya jua:Nikaona machozi ya walioonewa,wala hawana wa kuwafariji;uwezo ulikuwa upande wa wale wanaowaonea,wala hawana wa kuwafariji.

2Nami nikasema kwamba wafu,waliokwisha kufa,wana furaha kuliko watu walio hai,ambao bado wanaishi.

3Lakini aliye bora kuliko hao wawilini yule ambaye hajazaliwa bado,ambaye hajaona ule uovuunaofanyika chini ya jua.

4Tena nikaona kuwa kazi zote na mafanikio yote huchipuka kutokana na wivu wa mtu kwa jirani yake. Hili nalo ni ubatili, ni kukimbiza upepo.

5Mpumbavu hukunja mikono yakena kujiangamiza mwenyewe.

6Afadhali konzi moja pamojana utulivu kuliko konzi mbili pamoja na taabu
na kukimbiza upepo.

7Tena nikaona kitu kingine kilicho ubatili chini ya jua:

8Kulikuwepo mwanadamu aliye peke yake,hakuwa na mwana wala ndugu.Hapakuwa na mwisho wa kazi yake,hata hivyo macho yake
hayakutosheka na utajiri wake.Aliuliza, “Ninajitaabisha hivi kwa ajili ya nani,nami kwa nini ninajinyima kufurahia?”Hili pia ni ubatili,ni shughuli yenye taabu!

9Wawili ni afadhali kuliko mmoja,kwa sababu wana malipo mazuri kwa kazi yao:

10Kama mmoja akianguka,mwenzake atamwinua.Lakini ni jambo la kuhuzunishakwa mtu yule aangukaye
naye hana wa kumwinua!

11Pia, kama wawili wakilala pamojawatapashana joto.Lakini ni vipi mtu awezakujipasha joto mwenyewe?

12Ingawa mtu mmoja aweza kushindwa,watu wawili wanaweza
kumkabili adui na kumshinda.Kamba ya nyuzi tatuhaikatiki kwa urahisi.

Maendeleo Ni Ubatili

13Afadhali kijana maskini mwenye hekima kuliko mfalme mzee mpumbavu ambaye hajui tena kupokea maonyo.

14Kijana huyo angeweza kutokea gerezani akapata ufalme, au angeweza kuwa amezaliwa katika umaskini kwenye huo ufalme.

15Nikaona kwamba wote walioishi na kutembea chini ya jua walimfuata kijana, aliyepokea ufalme.

16Hapakuwa na kikomo cha watu wote aliowatawala. Lakini wale waliokuja baadaye hawakufurahia kazi ya yule aliyepokea ufalme. Hili nalo pia ni ubatili, ni kukimbiza upepo.