Inapakia...
📖

Biblia Takatifu

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™
BIB 14 mistari

Ezekieli 19

Ezekieli • Sura 19 / 48

Maombolezo Kwa Ajili Ya Wakuu Wa Israeli

1“Wewe fanya maombolezo kuhusu wakuu wa Israeli

2na useme:“ ‘Tazama jinsi gani mama yako alivyokuwa simba jikemiongoni mwa simba!Alilala katikati ya wana simbana kulisha watoto wake.

3Alimlea mmoja wa watoto wake,naye akawa simba mwenye nguvu.Akajifunza kurarua mawindonaye akala watu.

4Mataifa wakasikia habari zake,naye akanaswa katika shimo lao.Wakamwongoza kwa ndoanampaka nchi ya Misri.

5“ ‘Mama yake alipongoja na kuona tumaini lake halitimiziki,nayo matarajio yake yametoweka,akamchukua mwanawe mwinginena kumfanya simba mwenye nguvu.

6Alizungukazunguka miongoni mwa simba,kwa kuwa sasa alikuwa simba mwenye nguvu.Akajifunza kurarua mawindonaye akala watu.

7Akabomoa ngome zaona kuiharibu miji yao.Nchi na wote waliokuwa ndani yakewakatiwa hofu kwa kunguruma kwake.

8Kisha mataifa wakaja dhidi yakekutoka sehemu zilizomzunguka.Wakatanda nyavu zao kwa ajili yake,naye akanaswa katika shimo lao.

9Kwa kutumia ndoana wakamvutia kwenye tunduna kumleta mpaka kwa mfalme wa Babeli.Wakamtia gerezani, hivyo kunguruma kwakehakukusikika tena
katika milima ya Israeli.

10“ ‘Mama yako alikuwa kama mzabibukatika shamba lako la mizabibu
uliopandwa kando ya maji,ukiwa unazaa sana na wenye matawi mengikwa sababu ya wingi wa maji.

11Matawi yake yalikuwa na nguvu,yaliyofaa kuwa fimbo ya enzi ya mtawala.Ulikuwa mrefu kupita miti minginekatikati ya matawi manene;ulionekana kwa urahisikwa ajili ya urefu wake
na wingi wa matawi yake.

12Lakini ulingʼolewa kwa hasira kalina kutupwa chini.Upepo wa mashariki uliufanya usinyae,matunda yake yakapukutika,matawi yake yenye nguvu yakanyaukana moto ukayateketeza.

13Sasa umepandwa jangwanikatika nchi kame na ya kiu.

14Moto ulienea kuanzia katika mmojawapo ya matawi yake makubwana kuteketeza matunda yake.Hakuna tawi lenye nguvu lililobaki juu yakelifaalo kuwa fimbo ya enzi ya mtawala.’Hili ndilo ombolezo, na litumike kama ombolezo.”