Inapakia...
📖

Biblia Takatifu

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™
BIB 36 mistari

Ezekieli 27

Ezekieli • Sura 27 / 48

Maombolezo Kwa Ajili Ya Tiro

1Neno la Bwana likanijia kusema:

2“Mwanadamu, fanya maombolezo kwa ajili ya Tiro.

3Umwambie Tiro, ulioko kwenye lango la bahari, ufanyao biashara na mataifa mengi ya pwani, ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo:“ ‘Ee Tiro, wewe umesema,“Mimi ni mkamilifu katika uzuri.”

4Mipaka yako ilikuwa katika moyo wa bahari,wajenzi wako walikamilisha uzuri wako.

5Walizifanya mbao zako zotekwa misunobari itokayo Seniri;*walichukua mierezi kutoka Lebanonikukutengenezea mlingoti.

6Walichukua mialoni toka Bashaniwakakutengenezea makasia yako;kwa miti ya msandukukutoka pwani ya Kitimuwakatengeneza sitaha*yakona kuipamba kwa pembe za ndovu.

7Kitani safi kilichotariziwa kutoka Misri kilikuwa tanga lako,nacho kilikuwa bendera yako;chandarua chako kilikuwa cha rangi ya buluu na ya zambaraukutoka visiwa vya Elisha.

8Watu kutoka Sidoni na Arvadi walikuwa wapiga makasia yako;watu wako wenye ustadi, ee Tiro,
walikuwa ndio mabaharia wako.

9Wazee wa Gebali*pamoja na mafundi stadiwalikuwa mafundi wako melini.Meli zote za baharini na mabaharia waowalikuja kwako ili kubadilishana bidhaa zako.

10“ ‘Watu wa Uajemi, Ludi na Putuwalikuwa askari katika jeshi lako.Walitundika ngao zao na chapeo zao kwenye kuta zako,wakileta fahari yako.

11Watu wa Arvadi na wa Helekiwalikuwa juu ya kuta zako pande zote;watu wa Gamadiwalikuwa kwenye minara yako.Walitundika ngao zao kuzizunguka kuta zako;wakaukamilisha uzuri wako.

12“ ‘Tarshishi walifanya biashara nawe kwa sababu ya utajiri wako mkubwa wa bidhaa, walibadilisha fedha, chuma, bati na risasi kwa mali zako.

13“ ‘Uyunani, Tubali na Mesheki, walifanya biashara nawe, walibadilisha watumwa na vyombo vya shaba kwa bidhaa zako.

14“ ‘Watu wa Beth-Togarma walibadilisha farasi wa mizigo, farasi wa vita na nyumbu kwa mali zako.

15“ ‘Watu wa Dedani*walifanya biashara nawe, watu wengi wa nchi za pwani walikuwa wachuuzi wako, walikulipa kwa pembe za ndovu na mpingo.

16“ ‘Watu wa Aramu walifanya biashara nawe kwa ajili ya wingi wa kazi za mikono yako, wakibadilishana kwa almasi, vitambaa vya rangi ya zambarau, vitambaa vilivyotariziwa, kitani safi, matumbawe*na akiki nyekundu.

17“ ‘Yuda na Israeli walifanya biashara nawe, walibadilishana kwa ngano kutoka Minithi, mtama, asali, mafuta na zeri ya kuponyeshea.

18“ ‘Dameski, kwa sababu ya wingi wa kazi za mikono yako na ukuu wa utajiri wa mali, walifanya biashara nawe wakibadilishana mvinyo kutoka Helboni na sufu kutoka Zahari.

19“ ‘Wadani na Wayunani kutoka Uzali, walikuletea mali za biashara, nao wakabadilishana nawe chuma kilichofuliwa, mdalasini na mchaichai.

20“ ‘Dedani alifanya biashara nawe kwa matandiko ya farasi.

21“ ‘Arabuni na wakuu wote wa Kedari walikuwa wanunuzi wako waliobadilishana bidhaa zako na wana-kondoo, kondoo dume na mbuzi.

22“ ‘Wafanyabiashara wa Sheba na wa Raama walifanya biashara nawe, wakabadilishana bidhaa zako na aina zote za vikolezi, vito vya thamani na dhahabu.

23“ ‘Harani, Kane na Edeni na wafanyabiashara wa Sheba, Ashuru na Kilmadi walifanya biashara nawe.

24Kwenye soko lako, walifanya biashara nawe kwa mavazi mazuri, vitambaa vya buluu, nguo za kutariziwa na mazulia ya rangi mbalimbali yenye kamba zilizosokotwa na kuwekwa mafundo imara.

25“ ‘Merikebu za Tarshishi ndizozinazokusafirishia bidhaa zako.Umejazwa shehena kubwakatika moyo wa bahari.

26Wapiga makasia wako wanakupelekampaka kwenye maji makavu.Lakini upepo wa mashariki umekuvunja vipande vipandekatika moyo wa bahari.

27Utajiri wako, bidhaa zako na mali zako,mabaharia wako, manahodha wako,
mafundi wako wa meli,wafanyabiashara wako na askari wako wote,na kila mmoja aliyeko meliniatazama kwenye moyo wa baharisiku ile ya kuvunjika kwa meli yako.

28Nchi za pwani zitatetemekawakati mabaharia wako watakapopiga kelele.

29Wote wapigao makasiawataacha meli zao,mabaharia wote na wanamaji wotewatasimama pwani.

30Watapaza sauti zaona kulia sana kwa ajili yako;watajitupia mavumbi juu ya vichwa vyaona kujivingirisha kwenye majivu.

31Watanyoa nywele zao kwa ajili yako,nao watavaa nguo za magunia.Watakulilia kwa uchungu wa moyona kwa maombolezo makuu.

32Watakapokuwa wanalia na kuomboleza juu yako,watafanya maombolezo kukuhusu wakisema:“Ni nani aliyepata kuangamizwa kama Tiro,katika moyo wa bahari?”

33Wakati bidhaa zako zilipotoka baharini,ulitosheleza mataifa mengi;kwa wingi wa utajiri wako na bidhaa zakoulitajirisha wafalme wa dunia.

34Sasa umevunjavunjwa na bahari,katika vilindi vya maji,bidhaa zako na kundi lako lotevimezama pamoja nawe.

35Wote waishio katika nchi za pwaniwanakustaajabia;wafalme wao wanatetemeka kwa hofu kuu,nazo nyuso zao zimekunjamana kwa woga.

36Wafanyabiashara miongoni mwa mataifa wanakucheka;umefikia mwisho wa kutisha
nawe hutakuwepo tena.’ ”

Tanbihi

*

Yaani Hermoni.

*

Yaani sakafu ya merikebu au mashua.

*

Yaani Bubilo, mji wa zamani sana wa Ufoinike (kama kilomita 80 kaskazini mwa Beiruti).

*

Yaani Rhodes.

*

Yaani marijani, jiwe laini la pwani au baharini, kama mawe ya chokaa.