Inapakia...
📖

Biblia Takatifu

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™
BIB 70 mistari

Ezra 2

Ezra • Sura 2 / 10

Orodha Ya Watu Waliorudi Kutoka Uhamishoni

1Basi hawa ndio watu wa jimbo waliotoka uhamishoni, ambao Nebukadneza mfalme wa Babeli alikuwa amewachukua mateka hadi Babeli (walirudi Yerusalemu na Yuda, kila mmoja kwenye mji wake,

2wakiwa wamefuatana na Zerubabeli, Yeshua, Nehemia, Seraya, Reelaya, Mordekai, Bilshani, Mispari, Bigwai, Rehumu na Baana):
Orodha ya wanaume kati ya watu wa Israeli ilikuwa:

3wazao wa Paroshi2,172

4wazao wa Shefatia372

5wazao wa Ara775

6wazao wa Pahath-Moabu (wa jamaa ya Yeshua na Yoabu)2,812

7wazao wa Elamu1,254

8wazao wa Zatu945

9wazao wa Zakai760

10wazao wa Bani642

11wazao wa Bebai623

12wazao wa Azgadi1,222

13wazao wa Adonikamu666

14wazao wa Bigwai2,056

15wazao wa Adini454

16wazao wa Ateri (kupitia Hezekia)98

17wazao wa Besai323

18wazao wa Yora112

19wazao wa Hashumu223

20wazao wa Gibari95

21watu wa Bethlehemu123

22watu wa Netofa56

23watu wa Anathothi128

24watu wa Azmawethi42

25wazao wa Kiriath-Yearimu, Kefira na Beerothi743

26wazao wa Rama na Geba621

27watu wa Mikmashi122

28watu wa Betheli na Ai223

29wazao wa Nebo52

30wazao wa Magbishi156

31wazao wa Elamu ile ingine1,254

32wazao wa Harimu320

33wazao wa Lodi, Hadidi na Ono725

34wazao wa Yeriko345

35wazao wa Senaa3,630

36Makuhani: wazao wa Yedaya (kwa jamaa ya Yeshua)973

37wazao wa Imeri1,052

38wazao wa Pashuri1,247

39wazao wa Harimu1,017

40Walawi: wazao wa Yeshua na Kadmieli (kupitia jamaa ya Hodavia)74

41Waimbaji: wazao wa Asafu128

42Mabawabu wa lango la Hekalu: wazao waShalumu, Ateri, Talmoni,Akubu, Hatita na Shobai139

43Watumishi wa Hekalu:*wazao wa Siha, Hasufa, Tabaothi,

44wazao wa Kerosi, Siaha, Padoni,

45wazao wa Lebana, Hagaba, Akubu,

46wazao wa Hagabu, Shalmai, Hanani,

47wazao wa Gideli, Gahari, Reaya,

48wazao wa Resini, Nekoda, Gazamu,

49wazao wa Uza, Pasea, Besai,

50wazao wa Asna, Meunimu, Nefusimu,

51wazao wa Bakbuki, Hakufa, Harhuri,

52wazao wa Basluthi, Mehida, Harsha,

53wazao wa Barkosi, Sisera, Tema,

54wazao wa Nesia na Hatifa.

55Wazao wa watumishi wa Solomoni: wazao wa Sotai, Hasaferethi, Peruda,

56wazao wa Yaala, Darkoni, Gideli,

57wazao wa Shefatia, Hatili, Pokereth-Hasebaimu na Ami.

58Watumishi wa Hekalu wote nawazao wa watumishiwa Solomoni392

59Wafuatao walikuja kutoka miji ya Tel-Mela, Tel-Harsha, Kerubu, Adoni na Imeri, lakini hawakuweza kuthibitisha kwamba jamaa zao zilikuwa uzao wa Israeli:

60wazao waDelaya, Tobia na Nekoda652

61Kutoka miongoni mwa makuhani: Wazao wa Hobaya, Hakosi, Barzilai (mtu aliyekuwa amemwoa binti wa Barzilai, Mgileadi, naye akaitwa kwa jina hilo).

62Hawa walitafuta orodha za jamaa zao, lakini hawakuonekana humo, kwa hiyo waliondolewa kutoka kundi la makuhani kwa kuwa walihesabiwa kuwa najisi.

63Mtawala aliagiza kuwa wasile chochote miongoni mwa vyakula vitakatifu hadi kuwe kuhani atakayehudumu kwa Urimu na Thumimu.*

64Jumla ya watu wote waliorudi walikuwa 42,360;

65tena zaidi ya hao walikuwepo watumishi wa kiume na wa kike 7,337; pia walikuwamo waimbaji wanaume na wanawake 200.

66Walikuwa na farasi 736, nyumbu 245,

67ngamia 435 na punda 6,720.

68Walipofika kwenye nyumba ya Bwana huko Yerusalemu, baadhi ya viongozi wa jamaa walitoa sadaka za hiari kwa ajili ya kujenga upya nyumba ya Mungu katika eneo lake.

69Wakatoa kwa kadiri ya uwezo wao na kutia katika hazina darkoni 61,000*za dhahabu, mane 5,000*za fedha, na mavazi 100 ya ukuhani kwa ajili ya kazi hiyo.

70Makuhani, Walawi, waimbaji, mabawabu, na watumishi wa Hekalu waliishi katika miji yao wenyewe, pamoja na baadhi ya watu wengine, nao Waisraeli waliosalia waliishi katika miji yao.

Tanbihi

*

Yaani Wanethini (pia 2:58, 70).

*

Urimu na Thumimu maana yake ni Nuru na Kweli; vifaa hivi viliwekwa kwenye kifuko cha kifuani cha kisibau cha kuhani mkuu ili kujua mapenzi ya Mungu kwenye mambo ya kutatanisha.

*

Darkoni 61,000 za dhahabu ni sawa na kilo 500.

*

Mane 5,000 za fedha ni sawa na kilo 2,900.