Inapakia...
📖

Biblia Takatifu

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™
BIB 14 mistari

Hosea 12

Hosea • Sura 12 / 14

1Efraimu anajilisha upepo;hufukuzia upepo wa mashariki kutwa nzima
na kuzidisha uongo na jeuri.Anafanya mkataba na Ashuruna kutuma mafuta ya zeituni Misri.

2Bwana analo shtaka dhidi ya Yuda,atamwadhibu Yakobo kwa kadiri ya njia zake
na kumlipa kwa kadiri ya matendo yake.

3Yakobo akiwa tumboni alishika kisigino cha kaka yake;kama mwanadamu, alishindana na Mungu.

4Alishindana na malaika na kumshinda;alilia na kuomba upendeleo wake.Alimkuta huko Bethelina kuzungumza naye huko:

5Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote,Bwana ndilo jina lake!

6Lakini ni lazima urudi kwa Mungu wako;dumisha upendo na haki,
nawe umngojee Mungu wako siku zote.

7Mfanyabiashara hutumia vipimo vya udanganyifu;hupenda kupunja.

8Efraimu hujisifu akisema,“Mimi ni tajiri sana; nimetajirika.Pamoja na utajiri wangu wote hawatakuta ndani yanguuovu wowote au dhambi.”

9“Mimi ndimi Bwana Mungu wenuniliyewaleta kutoka Misri;nitawafanya mkae tena kwenye mahema,kama vile katika siku
za sikukuu zenu zilizoamriwa.

10Niliongea na manabii, nikawapa maono mengina kusema mifano kupitia wao.”

11Je, Gileadi si mwovu?Watu wake hawafai kitu!Je, hawatoi dhabihu za mafahali huko Gilgali?Madhabahu zao zitakuwa
kama malundo ya mawe
katika shamba lililolimwa.

12Yakobo alikimbilia katika nchi ya Aramu;Israeli alitumika ili apate mke,
ili aweze kulipa kwa ajili yake alichunga kondoo.

13Bwana alimtumia nabiikumpandisha Israeli kutoka Misri,
kwa njia ya nabii alimtunza.

14Lakini Efraimu amemchochea sana hasira;Bwana wake ataleta juu yakehatia yake ya kumwaga damu naye atamlipizakwa ajili ya dharau yake.