1âWaambie ndugu zako, âWatu wangu,â na pia waambie dada zako, âWapendwa wangu.â
2âMkemeeni mama yenu, mkemeeni,kwa maana yeye si mke wangu,
nami si mume wake.Aondoe sura ya uzinzi katika uso wakena uzinzi kati ya matiti yake.
3Kama sivyo nitamvua nguo zake awe uchina kumwacha uchi kama siku ile aliyozaliwa.Nitamfanya kama jangwa,nitamgeuza awe nchi ya kiu,
nami nitamuua kwa kiu.
4Sitaonyesha upendo wangu kwa watoto wake,kwa sababu ni watoto wa uzinzi.
5Mama yao amekosa uaminifuna amewachukua mimba katika aibu.Gomeri alisema, âNitawaendea wapenzi wangu,ambao hunipa chakula changu
na maji yangu,sufu yangu na kitani yangu, mafuta yanguna kinywaji changu.â
6Kwa hiyo mimi Mungu nitaizuia njia yakekwa vichaka vya miiba,nitamjengea ukuta ili kwambaasiweze kutoka.
7Gomeri atawafuatia wapenzi wake lakini hatawapata;atawatafuta lakini hatawapata.Kisha atasema,âNitarudi kwa mume wangu kama kwanza,kwa maana nilikuwa na hali njema zaidikuliko sasa.â
8Gomeri hajakubali kuwa mimi ndiyeniliyempa nafaka, divai mpya na mafuta,niliyemwongezea fedha na dhahabu waliyoitumiakwa kumtumikia Baali.
9âKwa hiyo nitachukua nafaka yangu wakati itakapokomaana divai yangu mpya wakati itakapokuwa tayari.NitamnyangĘźanya sufu yangu na kitani yanguiliyokusudiwa kufunika uchi wake.
10Basi sasa nitaufunua ufisadi wakembele ya wapenzi wake;hakuna yeyote atakayemtoamikononi mwangu.
11Nitakomesha furaha na macheko yake yote:sikukuu zake za mwaka,
sikukuu za Miandamo ya Mwezi,
siku zake za Sabato,
sikukuu zake zote zilizoamriwa.
12Nitaiharibu mizabibu yake na mitini yake,ambayo alisema yalikuwa malipo yake
kutoka kwa wapenzi wake;nitaifanya kuwa kichaka,nao wanyama pori wataila.
13Nitamwadhibu kwa ajili ya sikualizowafukizia uvumba Mabaali;alipojipamba kwa petena kwa vito vya thamani,na kuwaendea wapenzi wake,lakini mimi alinisahau,âasema Bwana.
14âKwa hiyo sasa nitamshawishi;nitamwongoza hadi jangwani
na kuzungumza naye kwa upole.
15Huko nitamrudishia mashamba yake ya mizabibu,nami nitalifanya Bonde la Akori*
mlango wa matumaini.Huko ataimba kama alivyofanya katika siku za ujana wake,kama siku zile alizotoka Misri.
16âKatika siku ile,â asema Bwana,âutaniita mimi âMume wanguâ;
hutaniita tena mimi âBwana wangu.â
17Nitaondoa majina ya Mabaali kutoka midomoni mwake,wala hataomba tena kwa majina yao.
18Katika siku ile nitafanya Agano kwa ajili yaona wanyama wa kondeni, na ndege wa angani,
na viumbe vile vitambaavyo ardhini.Upinde, upanga na vita,nitaondolea mbali katika nchi,
ili kwamba wote waweze kukaa salama.
19Nitakuposa uwe wangu milele;nitakuposa kwa uadilifu na haki,
kwa upendo na huruma.
20Nitakuposa kwa uaminifu,nawe utamkubali Bwana.
21âKatika siku ile nitajibu,âasema Bwana,ânitajibu kwa anga,nazo anga zitajibu kwa nchi;
22nayo nchi itajibu kwa nafaka,divai mpya na mafuta,
navyo vitajibu kwa Yezreeli.
23Nitampanda katika nchi kwa ajili yangu mwenyewe;nami nitaonyesha pendo langu kwake
yule ambaye nilimwita, âSi mpenzi wangu.*âNitawaambia wale walioitwa, âSio watu wangu,â*âNinyi ni watu wanguâ;
nao watasema, âWewe ndiwe Mungu wangu.â â
Tanbihi
Akori maana yake ni Taabu.
Kiebrania ni Lo-Ruhama.
Kiebrania ni Lo-Ami.