1Neno kuhusu Misri:Tazama, Bwana amepanda juu ya wingu liendalo kwa harakanaye anakuja Misri.Sanamu za Misri zinatetemeka mbele yake,nayo mioyo ya Wamisri inayeyuka ndani yao.
2āNitamchochea Mmisri dhidi ya Mmisri,ndugu atapigana dhidi ya ndugu,
jirani dhidi ya jirani,
mji dhidi ya mji,
ufalme dhidi ya ufalme.
3Wamisri watakufa moyo,na nitaibatilisha mipango yao.Watatafuta ushauri kwa sanamu na kwa roho za waliokufa,kwa waaguzi na kwa wale waongeao na mizimu.
4Nitawatia Wamisrimikononi mwa bwana mkatilina mfalme mkali atatawala juu yao,āasema Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote.
5Maji ya mito yatakauka,chini ya mto kutakauka kwa jua.
6Mifereji itanuka;vijito vya Misri vitapungua
na kukauka.Mafunjo na nyasi vitanyauka,
7pia mimea iliyoko kando ya Mto Naili,
pale mto unapomwaga maji baharini.Kila shamba lililopandwa kando ya Mto Naili litakauka,litapeperushwa na kutoweka kabisa.
8Wavuvi watalia na kuomboleza,wale wote watupao ndoano katika Mto Naili,
watadhoofika kwa majonzi.
9Wale watu wafanyao kazi ya kitani kilichochambuliwa watakata tamaa,wafumaji wa kitani safi watavunjika moyo.
10Wafanyao kazi ya kufuma nguo watahuzunishwa,nao vibarua wataugua moyoni.
11Maafisa wa Soani ni wapumbavu kabisa,washauri wa Farao wenye busara wanatoa ushauri wa kijinga.Unawezaje kumwambia Farao,āMimi ni mmojawapo wa watu wenye hekima,
mwanafunzi wa wafalme wa zamaniā?
12Wako wapi sasa watu wako wenye hekima?Wao wakuonyeshe na kukufahamishani nini Bwana Mwenye Nguvu Zoteamepanga dhidi ya Misri.
13Maafisa wa Soani wamekuwa wapumbavu,viongozi wa Memfisi*wamedanganyika,walio mawe ya pembe ya taifa lakewameipotosha Misri.
14Bwana amewamwagiaroho ya kizunguzungu;wanaifanya Misri iyumbayumbekatika yale yote inayoyafanya,kama vile mlevi ayumbayumbavyokatika kutapika kwake.
15Misri haiwezi kufanya kitu chochote,cha kichwa wala cha mkia,
cha tawi la mtende wala cha tete.
16Katika siku ile Wamisri watakuwa kama wanawake. Watatetemeka kwa hofu mbele ya mkono wa Bwana Mwenye Nguvu Zote anaoinua dhidi yao.
17Nayo nchi ya Yuda itawatia hofu Wamisri, kila mmoja atakayetajiwa Yuda ataingiwa na hofu, kwa sababu ya kile ambacho Bwana Mwenye Nguvu Zote anapanga dhidi yao.
18Katika siku hiyo miji mitano ya Misri, itazungumza lugha ya Kanaani, na kuapa kumtii Bwana Mwenye Nguvu Zote. Mji mmojawapo utaitwa Mji wa Uharibifu.*
19Katika siku hiyo patakuwepo madhabahu ya Bwana katikati ya Misri na mnara wa kumbukumbu kwa Bwana kwenye mpaka wa Misri.
20Itakuwa alama na ushahidi kwa ajili ya Bwana Mwenye Nguvu Zote katika nchi ya Misri. Watakapomlilia Bwana kwa sababu ya watesi wao, Mungu atawapelekea mwokozi na mtetezi, naye atawaokoa.
21Hivyo Bwana atajijulisha mwenyewe kwa Wamisri, nao katika siku hiyo watamkubali Bwana. Wataabudu kwa kumtolea dhabihu na sadaka za nafaka, watamwekea Bwana nadhiri na kuzitimiza.
22Bwana ataipiga Misri kwa tauni; atawapiga na kuwaponya. Watamgeukia Bwana, naye atayasikia maombi yao na kuwaponya.
23Katika siku hiyo kutakuwepo na njia kuu kutoka Misri hadi Ashuru. Waashuru watakwenda Misri, na Wamisri watakwenda Ashuru. Wamisri na Waashuru wataabudu pamoja.
24Katika siku hiyo Israeli itakuwa ya tatu, pamoja na Misri na Ashuru, nao watakuwa baraka kwa dunia.
25Bwana Mwenye Nguvu Zote atawabariki, akisema, āBaraka iwe kwa Misri watu wangu, kwa Ashuru kazi ya mikono yangu, na kwa Israeli urithi wangu.ā
Tanbihi
Memfisi kwa Kiebrania ni Nofu.
Yaani Heliopoli (Mji wa Jua).