Inapakia...
📖

Biblia Takatifu

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™
BIB • 29 mistari

Isaya 28

Isaya • Sura 28 / 66

Ole Wa Efraimu

1Ole kwa lile taji la maua, kiburi cha walevi wa Efraimu,kwa ua linalosinyaa, uzuri wa utukufu wake,uliowekwa kwenye kichwa cha bonde lenye rutuba:kwa ule mji, kiburi cha wale walioshushwa na mvinyo!

2Tazama, Bwana anaye mmoja aliye na uwezo na nguvu.Kama dhoruba ya mvua ya mawe na upepo uharibuo,kama mvua inyeshayo kwa nguvu na mafuriko yashukayo,atakiangusha chini kwa nguvu.

3Lile taji la maua, kiburi cha walevi cha Efraimu,kitakanyagwa chini ya nyayo.

4Lile ua linalosinyaa, uzuri wa utukufu wake,uliowekwa kwenye kichwa cha bonde lenye rutuba,litakuwa kama tini iliyoiva kabla ya mavuno:mara mtu aionapo, huichuma na kuila.

5Katika siku ile, Bwana Mwenye Nguvu Zoteatakuwa taji la utukufu,taji zuri la mauakwa mabaki ya watu wake.

6Atakuwa roho ya hakikwa yeye aketiye katika kiti cha hukumu,chanzo cha nguvukwa wale wazuiao vita langoni.

7Hawa pia wanapepesuka kwa sababu ya mvinyo,wanayumbayumba kwa sababu ya kileo:Makuhani na manabii wanapepesuka kwa sababu ya kileo,wanachanganyikiwa kwa sababu ya mvinyo;wanapepesuka wanapoona maono,wanajikwaa wanapotoa maamuzi.

8Meza zote zimejawa na matapishiwala hakuna sehemu hata ndogo
isiyokuwa na uchafu.

9“Yeye anajaribu kumfundisha nani?Yeye anamwelezea nani ujumbe wake?Je, ni kwa watoto walioachishwa kunyonya?Je, ni wale ambao ndipo tu wametolewa matitini?

10Kwa maana ni:Amri juu ya amri, amri juu ya amri,
kanuni juu ya kanuni, kanuni juu ya kanuni;
hapa kidogo, kule kidogo.”

11Sawa kabisa, kwa midomo migenina kwa lugha ngeni,
Mungu atasema na watu hawa,

12wale ambao aliwaambia,“Hapa ni mahali pa kupumzika,
waliochoka na wapumzike,”na, “Hapa ni mahali pa mapumziko,”lakini hawakutaka kusikiliza.

13Hivyo basi, neno la Bwana kwao litakuwa:Amri juu ya amri, amri juu ya amri,
kanuni juu ya kanuni, kanuni juu ya kanuni,
hapa kidogo, kule kidogo:ili waende na kuanguka chali,wakijeruhiwa, wakinaswa na kukamatwa.

14Kwa hiyo sikieni neno la Bwana, enyi watu wenye dharaumnaotawala watu hawa wa Yerusalemu.

15Ninyi mnajisifu, “Tumefanya agano na mauti,tumefanya mapatano na kuzimu.Wakati pigo lifurikalo litakapopita,haliwezi kutugusa sisi,kwa kuwa tumefanya uongo kuwa kimbilio letuna miungu ya uongo kuwa mahali petu pa kujificha.”

16Kwa hiyo hivi ndivyo Bwana Mwenyezi asemavyo:“Tazama, ninaweka jiwe katika Sayuni,jiwe lililojaribiwa,jiwe la pembeni la thamani kwa ajili ya msingi thabiti.Yeye atumainiye kamwe hatatiwa hofu.

17Nitaifanya haki kuwa kamba ya kupimiana uadilifu kuwa timazi;mvua ya mawe itafagia kimbilio lenu, huo uongo,nayo maji yatafurikia mahali penu pa kujificha.

18Agano lenu na kifo litabatilishwa,patano lenu na kuzimu halitasimama.Wakati pigo lifurikalo litakapowakumba,litawaangusha chini.

19Kila mara lijapo litawachukua,asubuhi baada ya asubuhi,wakati wa mchana na wakati wa usiku,litawakumba tangu mwanzo hadi mwisho.”
Kuuelewa ujumbe huuutaleta hofu tupu.

20Kitanda ni kifupi mno kujinyoosha juu yake,nguo ya kujifunikia ni nyembamba mno
mtu hawezi kujifunikia.

21Bwana atainuka kama alivyofanya kwenye Mlima Perasimu,ataghadhibika kama alivyofanya katika Bonde la Gibeoni:ili kufanya kazi yake, kazi yake ya ajabu,ili kutimiza kazi yake, kazi yake ngeni.

22Sasa acheni dharau zenu,la sivyo minyororo yenu itakuwa mizito zaidi.Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote, ameniambiahabari za maangamizi yaliyoamriwa dhidi ya nchi yote.

23Sikilizeni msikie sauti yangu,tegeni masikio na msikie niyasemayo.

24Wakati mkulima alimapo ili apande,je, hulima siku zote?Je, huendelea kubomoa ardhina kusawazisha udongo?

25Akiisha kusawazisha shamba,je, hatapanyi mbegu za bizari na kutawanya jira?Je, hapandi ngano katika sehemu yake,shayiri katika eneo lake,
na nafaka nyingine katika shamba lake?

26Mungu wake humwelekezana kumfundisha njia iliyo sahihi.

27Iliki haipurwi kwa nyundo,wala gurudumu la gari halivingirishwi juu ya jira;iliki hupurwa kwa fimbo,na jira kwa ufito.

28Nafaka lazima isagwe ili kutengeneza mkate,kwa hiyo mtu haendelei kuipura daima.Ingawa huendesha magurudumu ya gari lake la kupuria juu yake,farasi wake hawasagi.

29Haya yote pia hutoka kwa Bwana Mwenye Nguvu Zote,mwenye mashauri ya ajabu, na anayepita wote kwa hekima.