1âLakini sasa sikiliza, ee Yakobo, mtumishi wangu,Israeli, niliyemchagua.
2Hili ndilo asemalo Bwana,yeye aliyekuhuluku, aliyekuumba tumboni,
yeye atakayekusaidia:Usiogope, ee Yakobo, mtumishi wangu,Yeshuruni,*niliyekuchagua.
3Kwa maana nitamimina maji juu ya nchi yenye kiu,na vijito vya maji juu ya ardhi iliyokauka;nitamimina Roho wangu juu ya watoto wako,nayo baraka yangu juu ya wazao wako.
4Nao watachipua kama manyasi katika shamba la majani,kama mierezi kando ya vijito vya maji yatiririkayo.
5Mmoja atasema, âMimi ni wa Bwanaâ;mwingine atajiita kwa jina la Yakobo;vilevile mwingine ataandika juu ya mkono wake, âWa Bwana,âna kujiita kwa jina la Israeli.
6âHili ndilo asemalo Bwana,Mfalme wa Israeli na Mkombozi,
Bwana Mwenye Nguvu Zote:Mimi ni wa kwanza na Mimi ni wa mwisho;zaidi yangu hakuna Mungu.
7Ni nani basi aliye kama mimi? Yeye na atangaze.Yeye atangaze na kuweka mbele yanguni kitu gani kilichotokea tangu nilipoumba watu wangu wa kale,tena ni nini kitakachotokea:
naam, yeye na atoe unabii ni nini kitakachokuja.
8Msitetemeke, msiogope.Je, sikutangaza hili, na kutoa unabii tangu zamani?Ninyi ni mashahidi wangu.Je, yuko Mungu zaidi yangu mimi?Hasha, hakuna Mwamba mwingine;mimi simjui mwingine.â
9Wote wachongao sanamu ni ubatili,navyo vitu wanavyovithamini havifai kitu.Wale ambao wanazitetea ni vipofu,ni wajinga, nao waaibika.
10Ni nani atengenezaye mungu na kusubu sanamu,ambayo haiwezi kumfaidia kitu chochote?
11Yeye pamoja na wenziwe wa aina yake wataaibishwa,mafundi wao si kitu ila ni wanadamu tu.Wote wakusanyike pamoja na kuwa na msimamo wao,watashushwa chini kwa hofu na kwa fedheha.
12Muhunzi huchukua kifaana kukifanyia kazi kwenye makaa ya moto,hutengeneza sanamu kwa nyundo,huifanyiza kwa nguvu za mkono wake.Huona njaa na kupoteza nguvu zake,asipokunywa maji huzimia.
13Seremala hupima kwa kutumia kambana huuchora mstari kwa kalamu;huchonga kwa patasina kutia alama kwa bikari.Huifanyiza katika umbo la binadamu,la mwanadamu katika utukufu wake wote,
ili iweze kukaa katika sehemu yake ya ibada ya miungu.
14Hukata miti ya mierezi,huchukua mtiriza au mwaloni.Huuacha ukue miongoni mwa miti ya msituni,au hupanda msunobari, nayo mvua huufanya ukue.
15Ni kuni ya binadamu:yeye huchukua baadhi yake na kuota moto,
huwasha moto na kuoka mkate.Lakini pia huutumia kumtengeneza mungu na akamwabudu,huitengeneza sanamu na kuisujudia.
16Sehemu ya kuni huziweka motoni,akapikia chakula chake,
hubanika nyama na kula hadi ashibe.Huota moto na kusema,âAha! Ninahisi joto, ninaona moto.â
17Mabaki yake hutengeneza mungu, sanamu yake;yeye huisujudia na kuiabudu.Huiomba na kusema,âNiokoe; wewe ni mungu wangu.â
18Hawajui chochote, hawaelewi chochote,macho yao yamefungwa hata hawawezi kuona,
akili zao zimefungwa hata hawawezi kufahamu.
19Hakuna anayefikiri,hakuna mwenye maarifa wala ufahamu wa kusema,âSehemu yake nilitumia kwa kuni;hata pia nilioka mkate juu ya makaa yake,
nikabanika nyama na kuila.Je, nifanye machukizo kwa kile kilichobaki?Je, nisujudie gogo la mti?â
20Hujilisha kwa majivu, moyo uliodanganyika humpotosha;hawezi kujiokoa mwenyewe, au kusema,
âJe, kitu hiki kilichoko katika mkono wangu wa kuume si ni uongo?â
21âEe Yakobo, kumbuka mambo haya,ee Israeli, kwa kuwa wewe ni mtumishi wangu.Nimekuumba wewe, wewe ni mtumishi wangu.Ee Israeli, sitakusahau.
22Nimeyafuta makosa yako kama wingu,dhambi zako kama ukungu wa asubuhi.Nirudie mimi,kwa kuwa nimekukomboa wewe.â
23Enyi mbingu, imbeni kwa furaha,kwa maana Bwana amefanya jambo hili.
Ee vilindi vya dunia, piga kelele.Enyi milima, pazeni sauti kwa nyimbo,enyi misitu na miti yenu yote,kwa maana Bwana amemkomboa Yakobo,ameuonyesha utukufu wake katika Israeli.
24âHili ndilo asemalo Bwana,Mkombozi wako, aliyekuumba tumboni:
âMimi ni Bwana,
niliyeumba vitu vyote,
niliyezitanda mbingu peke yangu,
niliyeitandaza nchi mwenyewe,
25âmimi huzipinga ishara za manabii wa uongo,na kuwatia upumbavu waaguzi,niyapinduaye maarifa ya wenye hekima,na kuyafanya kuwa upuzi,
26niyathibitishaye maneno ya watumishi wake,na kutimiza utabiri wa wajumbe wake,
âniambiaye Yerusalemu, âItakaliwa na watu,âniambiaye miji ya Yuda kuwa, âItajengwa,â
na kuhusu magofu yake, âMimi nitayatengeneza,â
27niambiaye kilindi cha maji, âKauka,nami nitakausha vijito vyako,â
28nisemaye kuhusu Koreshi, âYeye ni mchungaji wangu,naye atatimiza yote yanipendezayo;
atauambia Yerusalemu, âUkajengwe tena,â
na kuhusu Hekalu, âMisingi yake na iwekwe.â â
Tanbihi
Yeshuruni hapa maana yake ni Yeye aliye mnyofu, yaani Israeli (ona pia Kum 32:15).