Inapakia...
📖

Biblia Takatifu

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™
BIB 12 mistari

Isaya 62

Isaya • Sura 62 / 66

Jina Jipya La Sayuni

1Kwa ajili ya Sayuni sitanyamaza,kwa ajili ya Yerusalemu sitatulia,mpaka haki yake itakapoangaza kama mapambazuko,wokovu wake kama mwanga wa moto.

2Mataifa wataona haki yako,nao wafalme wote wataona utukufu wako;wewe utaitwa kwa jina jipyalile ambalo kinywa cha Bwana kitatamka.

3Utakuwa taji ya fahari mkononi mwa Bwana,taji ya kifalme mkononi mwa Mungu wako.

4Hawatakuita tena Aliyeachwa,wala nchi yako kuiita Ukiwa.Bali utaitwa Hefsiba,*nayo nchi yako itaitwa Beula,*kwa maana Bwana atakufurahia,nayo nchi yako itaolewa.

5Kama vile kijana aoavyo mwanamwali,ndivyo wanao*watakavyokuoa wewe;kama bwana arusi amfurahiavyo bibi arusi wake,ndivyo Mungu wako atakavyokufurahia wewe.

6Nimeweka walinzi juu ya kuta zako, ee Yerusalemu,hawatanyamaza mchana wala usiku.Ninyi wenye kumwita Bwana,msitulie,

7msimwache apumzike hadi atakapoufanya imara Yerusalemuna kuufanya uwe sifa ya dunia.

8Bwana ameapa kwa mkono wake wa kuumena kwa mkono wake wenye nguvu:“Kamwe sitawapa tena adui zenunafaka zenu kama chakula chao;kamwe wageni hawatakunywa tenadivai mpya ambayo mmeitaabikia,

9lakini wale waivunao nafaka watailana kumsifu Bwana,nao wale wakusanyao zabibu watainywa divai yakekatika nyua za patakatifu pangu.”

10Piteni, piteni katika malango!Tengenezeni njia kwa ajili ya watu.Jengeni, jengeni njia kuu!Ondoeni mawe.Inueni bendera kwa ajili ya mataifa.

11Bwana ametoa tangazompaka miisho ya dunia:“Mwambie Binti Sayuni,‘Tazama, mwokozi wako anakuja!Tazama ujira wake uko pamoja naye,na malipo yake yanafuatana naye!’ ”

12Wataitwa Watu Watakatifu,Waliokombolewa na Bwana;
nawe utaitwa Aliyetafutwa,
Mji Usioachwa Tena.

Tanbihi

*

Hefsiba maana yake Yeye ninayemfurahia.

*

Beula maana yake Aliyeolewa.

*

Au: wajenzi wako.