1Hili ndilo neno lililomjia Yeremia kutoka kwa Bwana:
2âSikia maneno ya agano hili, nawe uwaambie watu wa Yuda na wale waishio Yerusalemu.
3Waambie kwamba hili ndilo asemalo Bwana, Mungu wa Israeli: âAmelaaniwa mtu ambaye hatayatii maneno ya agano hili,
4maneno niliyowaamuru baba zenu nilipowatoa katika nchi ya Misri, kutoka tanuru la kuyeyushia vyuma.â Nilisema, âNitiini mimi na mfanye kila kitu ninachowaamuru, nanyi mtakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wenu.
5Kisha nitatimiza kiapo nilichowaapia baba zenu, kuwapa nchi itiririkayo maziwa na asali,â nchi ambayo mnaimiliki leo.â Nikajibu, âAmen, Bwana.â
6Bwana akaniambia, âTangaza maneno haya yote katika miji ya Yuda na katika barabara za Yerusalemu: âSikilizeni maneno ya agano hili na kuyafuata.
7Tangu wakati ule niliwapandisha baba zenu kutoka Misri mpaka leo, niliwaonya tena na tena, nikisema âNitiini mimi.â
8Lakini hawakusikiliza wala kujali. Badala yake, walifuata ukaidi wa mioyo yao miovu. Hivyo nikaleta juu yao laana zote za agano nililokuwa nimewaamuru wao kulifuata, lakini wao hawakulishika.â â
9Kisha Bwana akaniambia, âKuna shauri baya linaloendelea miongoni mwa watu wa Yuda na wale wanaoishi Yerusalemu.
10Wamerudia dhambi za baba zao, waliokataa kusikiliza maneno yangu. Wameifuata miungu mingine kuitumikia. Nyumba zote mbili za Israeli na Yuda zimelivunja agano nililofanya na baba zao.
11Kwa hivyo, hili ndilo asemalo Bwana: âNitaleta juu yao maafa ambayo hawawezi kuyakimbia. Hata kama wakinililia, sitawasikiliza.
12Miji ya Yuda na watu wa Yerusalemu watakwenda kuililia miungu ambayo wameifukizia uvumba, lakini haitawasaidia kamwe wakati maafa yatakapowapiga.
13Mnayo miungu mingi kama miji mliyo nayo, ee Yuda, nazo madhabahu mlizozijenga za kufukizia uvumba huyo mungu wa aibu Baali ni nyingi kama barabara za Yerusalemu.â
14âWewe usiwaombee watu hawa wala kufanya maombezi yoyote au kunisihi kwa ajili yao, kwa sababu sitawasikiliza watakaponiita wakati wa taabu yao.
15âMpenzi wangu anafanya nini hekaluni mwangu,anapofanya mashauri yake maovu na wengi?Je, nyama iliyowekwa wakfu yawezakuondolea mbali adhabu yako?Unapojiingiza katika ubaya wako,ndipo unashangilia.â
16Bwana alikuita mti wa mzeituni uliostawiulio na matunda mazuri kwa sura.Lakini kwa ngurumo ya mawimbi makuuatautia moto,
nayo matawi yake yatavunjika.
17Bwana Mwenye Nguvu Zote, aliyekupanda, ametamka maafa kwa ajili yako, kwa sababu nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda mmefanya maovu na kunikasirisha kwa kumfukizia Baali uvumba.
18Kwa sababu Bwana alinifunulia hila zao mbaya, nilizifahamu, kwa kuwa wakati ule alinionyesha yale waliyokuwa wanayafanya.
19Nilikuwa kama mwana-kondoo mpole aliyeongozwa machinjoni; mimi sikutambua kwamba walikuwa wamefanya shauri baya dhidi yangu, wakisema,âSisi na tuuangamize mti na matunda yake;nasi tumkatilie mbali kutoka nchi ya walio hai,
ili jina lake lisikumbukwe tena.â
20Lakini, Ee Bwana Mwenye Nguvu Zote, wewe uhukumuye kwa haki,nawe uchunguzaye moyo na akili,wacha nione ukiwalipiza wao kisasi,kwa maana kwako nimeweka shauri langu.
21âKwa hiyo hili ndilo Bwana asemalo kuhusu watu wa Anathothi wale wanaotafuta uhai wako wakisema, âUsitoe unabii kwa jina la Bwana, la sivyo utakufa kwa mikono yetuâ:
22kwa hiyo hili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote asemalo: âNitawaadhibu. Vijana wao waume watakufa kwa upanga, wana wao na binti zao kwa njaa.
23Hawatasaziwa hata mabaki kwao, kwa sababu nitaleta maafa kwa watu wa Anathothi katika mwaka wa adhabu yao.â â