Inapakia...
📖

Biblia Takatifu

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™
BIB 21 mistari

Yeremia 15

Yeremia • Sura 15 / 52

Adhabu Isiyoepukika

1Kisha Bwana akaniambia: “Hata kama Mose na Samweli wangesimama mbele zangu, moyo wangu usingewaelekea watu hawa. Waondoe mbele za macho yangu! Waache waende!

2Nao kama wakikuuliza, ‘Twende wapi?’ Waambie, ‘Hili ndilo Bwana asemalo:“ ‘Wale waliowekwa kwa ajili ya kufa, wakafe;waliowekwa kwa ajili ya upanga, kwa upanga;waliowekwa kwa ajili ya njaa, kwa njaa:waliowekwa kwa ajili ya kutekwa, watekwe.’ ”

3Bwana asema, “Nitatuma aina nne za waharabu dhidi yao: nazo ni upanga ili kuua na mbwa ili wakokote mbali, ndege wa angani na wanyama wa nchi ili kula na kuangamiza.

4Nitawafanya wawe machukizo kwa falme zote za dunia kwa sababu ya kile alichofanya Manase mwana wa Hezekia mfalme wa Yuda huko Yerusalemu.

5“Ni nani atakayekuhurumia, ee Yerusalemu?Ni nani atakayeomboleza kwa ajili yako?Ni nani atakayesimama ili kuulizakuhusu hali yako?

6Umenikataa mimi,” asema Bwana.“Unazidi kukengeuka.Hivyo nitanyoosha mkono wangu juu yako na kukuangamiza,siwezi kuendelea kukuonea huruma.

7Nitawapepeta kwa uma wa kupepeteakwenye malango ya miji katika nchi.Nitaleta msiba na maangamizi juu ya watu wangu,kwa maana hawajabadili njia zao.

8Nitawafanya wajane wao kuwa wengikuliko mchanga wa bahari.Wakati wa adhuhuri nitamleta mharabudhidi ya mama wa vijana wao waume;kwa ghafula nitaleta juu yaomaumivu makuu na hofu kuu.

9Mama mwenye watoto saba atazimiana kupumua pumzi yake ya mwisho.Jua lake litatua kungali bado mchana,atatahayarika na kufedheheka.Wale wote waliobaki nitawaua kwa upangambele ya adui zao,”asema Bwana.

10Ole wangu, mama yangu, kwamba ulinizaa,mtu ambaye ulimwengu wote
unashindana na kugombana naye!Sikukopa wala sikukopesha,lakini kila mmoja ananilaani.

11Bwana akasema,“Hakika nitakuokoa kwa kusudi jema,hakika nitawafanya adui zako wakuombe msaada
nyakati za maafa na nyakati za dhiki.

12“Je, mtu aweza kuvunja chuma,chuma kitokacho kaskazini, au shaba?

13Utajiri wako na hazina zako nitavitoa kuwa nyara,bila gharama,kwa sababu ya dhambi zako zotekatika nchi yako yote.

14Nitakufanya uwe mtumwa wa adui zakokatika nchi usiyoijua,kwa kuwa katika hasira yangu moto umewashwautakaowaka juu yako daima.”

15Wewe unafahamu, Ee Bwana,unikumbuke na unitunze mimi.
Lipiza kisasi juu ya watesi wangu.Kwa uvumilivu wako usiniondolee mbali;kumbuka jinsi ninavyoshutumiwa.

16Maneno yako yalipokuja, niliyala;yakawa shangwe yangu
na furaha ya moyo wangu,kwa kuwa nimeitwa kwa jina lako,Ee Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote.

17Kamwe sikuketi katika kundi la wafanyao sherehe,wala kamwe sikujifurahisha pamoja nao;niliketi peke yangu kwa sababu mkono wako ulikuwa juu yangu,na wewe ulikuwa umenijaza hasira.

18Kwa nini maumivu yangu hayakomi,na jeraha langu ni la kuhuzunisha,
wala haliponyeki?Je, utakuwa kwangu kama kijito cha udanganyifu,kama chemchemi iliyokauka?

19Kwa hiyo hili ndilo asemalo Bwana:“Kama ukitubu, nitakurejezaili uweze kunitumikia;kama ukinena maneno yenye maana,wala si ya upuzi,
utakuwa mnenaji wangu.Watu hawa ndio watakaokugeukia,wala si wewe utakayewageukia wao.

20Nitakufanya wewe uwe ukuta kwa watu hawa,ngome ya ukuta wa shaba;watapigana nawelakini hawatakushinda,kwa maana mimi niko pamoja nawekukuponya na kukuokoa,”asema Bwana.

21“Nitakuokoa kutoka mikono ya waovu,na kukukomboa kutoka makucha ya watu wakatili.”