1Hili ndilo neno lililomjia Yeremia kutoka kwa Bwana:
2âShuka uende mpaka nyumba ya mfinyanzi, nami huko nitakupa ujumbe wangu.â
3Kwa hiyo nikashuka mpaka kwenye nyumba ya mfinyanzi, nikamkuta akifinyanga kwa gurudumu lake.
4Lakini chombo alichokuwa akikifinyanga kutokana na udongo kilivunjika mikononi mwake, hivyo mfinyanzi akakifanya kuwa chombo kingine, umbo jingine kama vile ilivyoonekana vyema kwake yeye.
5Kisha neno la Bwana likanijia kusema:
6âEe nyumba ya Israeli, je, siwezi kuwafanyia kama huyu mfinyanzi afanyavyo?â asema Bwana. âKama vile udongo ulivyo katika mikono ya mfinyanzi, ndivyo mlivyo katika mkono wangu, ee nyumba ya Israeli.
7Ikiwa wakati wowote nikitangaza kuwa taifa au ufalme utangĘźolewa, utaangushwa na kuangamizwa,
8ikiwa lile taifa nililolionya litatubia uovu wake, ndipo nitakapokuwa na huruma, wala sitawapiga kwa maafa niliyokuwa nimewakusudia.
9Ikiwa wakati mwingine nitatangaza kuwa taifa ama utawala ujengwe na kuwekwa wakfu,
10ikiwa utafanya maovu mbele zangu na hukunitii, ndipo nitakapoghairi makusudio yangu mema niliyokuwa nimeyakusudia.
11âBasi kwa hiyo waambie watu wa Yuda na wale waishio Yerusalemu, âHili ndilo asemalo Bwana: Tazama! Ninaandaa maafa kwa ajili yenu, nami ninabuni mabaya dhidi yenu. Kwa hiyo geukeni kutoka njia zenu mbaya, kila mmoja wenu, tengenezeni njia zenu na matendo yenu.â
12Lakini wao watajibu, âHakuna faida. Tutaendelea na mipango yetu wenyewe, kila mmoja wetu atafuata ukaidi wa moyo wake mbaya.â â
13Kwa hiyo hili ndilo asemalo Bwana:âUlizia miongoni mwa mataifa:Ni nani alishasikia jambo kama hili?Jambo la kutisha sana limefanywana Bikira Israeli.
14Je, barafu ya Lebanoni iliwahi kutowekakwenye miteremko yake ya mawe wakati wowote?Je, maji yake baridi yatokayo katika vyanzo vilivyo mbaliyaliwahi kukoma kutiririka wakati wowote?
15Lakini watu wangu wamenisahau mimi,wanafukizia uvumba sanamu zisizofaa kitu,zilizowafanya wajikwae katika njia zaona katika mapito ya zamani.Zimewafanya wapite kwenye vichochorona kwenye barabara ambazo hazikujengwa.
16Nchi yao itaharibiwa,itakuwa kitu cha kudharauliwa daima;wote wapitao karibu nayo watashangaana kutikisa vichwa vyao.
17Kama upepo utokao mashariki,nitawatawanya mbele ya adui zao;nitawapa kisogo wala sio uso,katika siku ya maafa yao.â
18Wakasema, âNjooni, tutunge hila dhidi ya Yeremia; kwa kuwa kufundisha sheria kwa kuhani hakutapotea, wala shauri litokalo kwa mwenye hekima, wala neno la manabii. Hivyo njooni, tumshambulie kwa ndimi zetu na tusijali chochote asemacho.â
19Nisikilize, Ee Bwana,sikia wanayosema washtaki wangu!
20Je, mema yalipwe kwa mabaya?Lakini wao wamenichimbia shimo.Kumbuka kwamba nilisimama mbele yakona kunena mema kwa ajili yao,
ili wewe ugeuze hasira yako kali mbali nao.
21Kwa hiyo uwaache watoto wao waone njaa;uwaache wauawe kwa makali ya upanga.Wake zao wasiwe na watoto, na wawe wajane;waume wao wauawe,nao vijana wao waumewachinjwe kwa upanga vitani.
22Kilio na kisikike kutoka kwenye nyumba zaoghafula uwaletapo adui dhidi yao,kwa kuwa wamechimba shimo ili kunikamatana wameitegea miguu yangu mitego.
23Lakini unajua, Ee Bwana,hila zao zote za kuniua.Usiyasamehe makosa yaowala usifute dhambi zao
mbele za macho yako.Wao na waangamizwe mbele zako;uwashughulikie wakati wa hasira yako.