1Ikawa kuhani Pashuri mwana wa Imeri, mkuu wa maafisa wa Hekalu la Bwana, alipomsikia Yeremia akitoa unabii juu ya mambo haya,
2akaamuru Yeremia nabii apigwe na kufungwa kwenye mkatale katika Lango la Juu la Benyamini huko Hekaluni la Bwana.
3Siku ya pili Pashuri alipomwachia kutoka kwenye mkatale, Yeremia akamwambia, “Bwana hakukuita jina lako kuwa Pashuri bali Magor-Misabibu.*
4Kwa kuwa hili ndilo asemalo Bwana: ‘Nitakufanya kuwa hofu kuu kwako wewe mwenyewe na rafiki zako wote, na kwa macho yako mwenyewe utawaona wakianguka kwa upanga wa adui zao. Nitawatia Yuda wote mikononi mwa mfalme wa Babeli, ambaye atawachukua na kuwapeleka Babeli, ama awaue kwa upanga.
5Nitatia utajiri wote wa mji huu kwa adui zao: yaani mazao yao yote, vitu vyao vyote vya thamani, na hazina zote za wafalme wa Yuda. Watavitwaa kwa nyara na kuvipeleka Babeli.
6Nawe Pashuri pamoja na wote waishio katika nyumba yako mtakwenda uhamishoni Babeli. Mtafia humo na kuzikwa, wewe na rafiki zako wote ambao umewatabiria uongo.’ ”
7Ee Bwana, umenidanganya,nami nikadanganyika;wewe una nguvu kuniliko,nawe umenishinda.Ninadharauliwa mchana kutwa,kila mmoja ananidhihaki.
8Kila ninenapo, ninapiga kelelenikitangaza ukatili na uharibifu.Kwa hiyo neno la Bwana limeniletea matukanona mashutumu mchana kutwa.
9Lakini kama nikisema, “Sitamtajawala kusema tena kwa jina lake,”neno lake linawaka ndani ya moyo wangu kama moto,moto uliofungwa ndani ya mifupa yangu.Nimechoka sana kwa kulizuia ndani mwangu;kweli, siwezi kujizuia.
10Ninasikia minongʼono mingi,“Hofu iko pande zote!
Mshtakini! Twendeni tumshtaki!”Rafiki zangu wote wananisubiri niteleze,wakisema,“Labda atadanganyika;kisha tutamshinda
na kulipiza kisasi juu yake.”
11Lakini Bwana yu pamoja namikama shujaa mwenye nguvu;hivyo washtaki wangu watajikwaana kamwe hawatashinda.Watashindwa, nao wataaibika kabisa;kukosa adabu kwao hakutasahauliwa.
12Ee Bwana Mwenye Nguvu Zote,wewe umjaribuye mwenye haki
na kupima moyo na nia,hebu nione ukilipiza kisasi juu yao,kwa maana kwako
nimeliweka shauri langu.
13Mwimbieni Bwana!Mpeni Bwana sifa!Yeye huokoa uhai wa mhitajikutoka mikononi mwa waovu.
14Ilaaniwe siku niliyozaliwa!Nayo isibarikiwe ile siku
mama yangu aliyonizaa!
15Alaaniwe mtu yule aliyemletea baba yangu habari,yule aliyemfanya afurahi sana, akisema,“Mtoto amezaliwa kwako,tena mtoto wa kiume!”
16Mtu huyo na awe kama miji ileambayo Bwana Mungu
aliiangamiza bila huruma.Yeye na asikie maombolezo asubuhina kilio cha vita adhuhuri.
17Kwa sababu hakuniua nikiwa tumboni,hivyo mama yangu angekuwa kaburi langu,nalo tumbo lake la uzazilingebaki kuwa kubwa daima.
18Kwa nini basi nilitoka tumboniili kuona taabu na huzuni,
na kuzimaliza siku zangu katika aibu?
Tanbihi
Magor-Misabibu maana yake hapa ni Vitisho pande zote.