1Hili ndilo asemalo Bwana: âShuka kwenye jumba la kifalme la mfalme wa Yuda, utangaze ujumbe huu huko:
2âSikia neno la Bwana, ee mfalme wa Yuda, wewe uketiye kwenye kiti cha enzi cha Daudi: wewe, maafisa wako na watu wako mnaopitia malango haya.
3Hili ndilo Bwana asemalo: Tenda haki na adili. Mwokoe mkononi mwa mdhalimu yeye aliyetekwa nyara. Usimtendee mabaya wala ukatili mgeni, yatima au mjane, wala usimwage damu isiyo na hatia mahali hapa.
4Kwa kuwa ukiwa mwangalifu kushika maagizo haya, ndipo wafalme watakaokalia kiti cha enzi cha Daudi watakapoingia kupitia malango ya jumba hili la kifalme, wakiwa wamepanda magari na farasi, huku wakifuatana na maafisa wao na watu wao.
5Lakini kama hutayatii maagizo haya, asema Bwana, ninaapa kwa nafsi yangu kwamba jumba hili litakuwa gofu.â â
6Kwa kuwa hili ndilo Bwana asemalo kuhusu jumba la kifalme la mfalme wa Yuda:âIngawa uko kama Gileadi kwangu,kama kilele cha Lebanoni,hakika nitakufanya uwe kama jangwa,kama miji ambayo haijakaliwa na watu.
7Nitawatuma waharabu dhidi yako,kila mtu akiwa na silaha zake,nao watazikata boriti zako nzuri za mierezina kuzitupa motoni.
8âWatu kutoka mataifa mengi watapitia karibu na mji huu na kuulizana, âKwa nini Bwana amefanya jambo la namna hii juu ya mji huu mkubwa?â
9Nalo jibu litakuwa: âKwa sababu wameliacha agano la Bwana, Mungu wao, na wameabudu na kuitumikia miungu mingine.â â
10Usimlilie yeye aliyekufa, wala usimwombolezee;badala yake, afadhali umlilie kwa uchungu
yule aliyepelekwa uhamishoni,kwa sababu kamwe hatairudiawala kuiona tena nchi yake alikozaliwa.
11Kwa kuwa hili ndilo asemalo Bwana kuhusu Shalumu*mwana wa Yosia, aliyeingia mahali pa baba yake kuwa mfalme wa Yuda, lakini ameondoka mahali hapa: âYeye kamwe hatarudi tena.
12Atafia huko mahali walipompeleka kuwa mateka; hataiona tena nchi hii.â
13âOle wake yeye ajengaye jumba lake la kifalme kwa njia ya dhuluma,vyumba vyake vya juu kwa udhalimu,akiwatumikisha watu wa nchi yake pasipo malipo,bila kuwalipa kwa utumishi wao.
14Asema, âNitajijengea jumba kuu la kifalme,na vyumba vya juu vyenye nafasi kubwa.âHivyo anaweka ndani yake madirisha makubwa,huweka kuta za mbao za mierezi,
na kuipamba kwa rangi nyekundu.
15âJe, inakufanya kuwa mfalmehuko kuongeza idadi ya mierezi?Je, baba yako hakuwa na chakula na kinywaji?Alifanya yaliyo sawa na haki,
hivyo yeye akafanikiwa katika yote.
16Aliwatetea maskini na wahitaji,hivyo yeye akafanikiwa katika yote.Je, hiyo si ndiyo maana ya kunijua mimi?âasema Bwana.
17âLakini macho yako na moyo wako vimeelekezwa tukatika mapato ya udhalimu,kwa kumwaga damu isiyo na hatia,kwa uonevu na ukatili.â
18Kwa hiyo hili ndilo asemalo Bwana kuhusu Yehoyakimu mwana wa Yosia mfalme wa Yuda:âHawatamwombolezea wakisema:âOle, ndugu yangu! Ole, umbu langu!âHawatamwombolezea wakisema:âOle, bwana wangu! Ole, fahari yake!â
19Atazikwa maziko ya punda:ataburutwa na kutupwa
nje ya malango ya Yerusalemu.â
20âPanda Lebanoni ukapige kelele,sauti yako na isikike huko Bashani,piga kelele toka Abarimu,kwa kuwa wote waliojiunga nawe wameangamizwa.
21Nilikuonya wakati ulipojisikia kwamba uko salama,lakini ulisema, âMimi sitasikiliza!âHii imekuwa kawaida yako tangu ujana wako;hujanitii mimi.
22Upepo utawaondoa wachungaji wako wote,na wale ulioungana nao wataenda uhamishoni.Kisha utaaibika na kufedhehekakwa sababu ya uovu wako wote.
23Wewe uishiye Lebanoni,wewe uliyetulia kwenye majengo ya mierezi,tazama jinsi utakavyoombolezamaumivu makali yatakapokupata,maumivu kama yale ya mwanamkemwenye utungu wa kuzaa!
24âHakika kama niishivyo,â asema Bwana, âhata kama wewe, Yekonia*mwana wa Yehoyakimu mfalme wa Yuda, ungekuwa pete yangu ya muhuri katika mkono wangu wa kuume, bado ningekungĘźoa hapo.
25Nitakutia mikononi mwa wale wanaotafuta uhai wako, wale unaowaogopa, yaani Nebukadneza mfalme wa Babeli na kwa Wakaldayo.
26Nitakutupa mbali wewe na mama aliyekuzaa mwende katika nchi nyingine, ambayo hakuna hata mmoja wenu aliyezaliwa huko, nanyi mtafia huko.
27Kamwe hamtarudi katika nchi mliyotamani kuirudia.â
28Je, huyu mtu Yekonia ni chungu kilichodharauliwa,chungu kilichovunjika,
chombo kisichotakiwa na mtu yeyote?Kwa nini yeye na watoto wake watupwe nje kwa nguvu,na kutupwa kwenye nchi wasioijua?
29Ee nchi, nchi, nchi,sikia neno la Bwana!
30Hili ndilo Bwana asemalo:
âMwandike huyu mtu kama asiye na mtoto,mtu ambaye hatafanikiwa maisha yake yote,kwa maana hakuna mtoto wake atakayefanikiwa,wala kukaa kwenye kiti cha enzi cha Daudi
wala kuendelea kutawala katika Yuda.â
Tanbihi
Shalumu ndiye pia anaitwa Yehoahazi.
Yekonia au Konia ni jina jingine la Yehoyakini.