Inapakia...
📖

Biblia Takatifu

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™
BIB 24 mistari

Yeremia 30

Yeremia • Sura 30 / 52

Kurudishwa Kwa Israeli

1Hili ndilo neno lililomjia Yeremia kutoka kwa Bwana:

2“Hili ndilo asemalo Bwana, Mungu wa Israeli: ‘Andika katika kitabu maneno yote niliyonena na wewe.

3Siku zinakuja,’ asema Bwana, ‘nitakapowaleta watu wangu Israeli na Yuda kutoka uhamishoni, na kuwarudisha katika nchi niliyowapa baba zao ili kuimiliki,’ asema Bwana.”

4Haya ndiyo maneno Bwana aliyoyanena kuhusu Israeli na Yuda:

5“Hili ndilo asemalo Bwana:“ ‘Vilio vya woga vinasikika:hofu kuu, wala si amani.

6Ulizeni na mkaone:Je, mwanaume aweza kuzaa watoto?Kwa nini basi ninaona kila mwanaume mwenye nguvuameweka mikono yake tumbonikama mwanamke aliye na utungu wa kuzaa,kila uso ukigeuka rangi kabisa?

7Tazama jinsi ile siku itakavyokuwa ya kutisha!Hakutakuwa na nyingine mfano wake.Utakuwa wakati wa dhiki kwa Yakobo,lakini ataokolewa kutoka hiyo.

8“ ‘Katika siku ile,’ asema Bwana Mwenye Nguvu Zote,‘nitaivunja nira kutoka shingoni mwaona kuvipasua vifungo vyao;wageni hawatawafanya tena watumwa.

9Badala yake, watamtumikia Bwana, Mungu waona Daudi mfalme wao,
nitakayemwinua kwa ajili yao.

10“ ‘Hivyo usiogope, ee Yakobo mtumishi wangu,usifadhaike, ee Israeli,’asema Bwana.‘Hakika, nitakuokoa kutoka mbali,wazao wako kutoka nchi ya uhamisho wao.Yakobo atakuwa tena na amani na usalama,wala hakuna atakayemtia hofu.

11Mimi niko pamoja nawe, nami nitakuokoa,’asema Bwana.‘Ingawa nitayaangamiza kabisa mataifa yoteambamo miongoni mwao nimewatawanya,
sitawaangamiza ninyi kabisa.Nitawaadhibu, lakini kwa haki.Sitawaacha kabisa bila adhabu.’

12“Hili ndilo asemalo Bwana:“ ‘Kidonda chako hakina dawa,jeraha lako haliponyeki.

13Hakuna yeyote wa kukutetea shauri lako,hakuna dawa ya kidonda chako,
wewe hutapona.

14Wale walioungana nawe wote wamekusahau,hawajali chochote kukuhusu wewe.Nimekupiga kama vile adui angelifanya,na kukuadhibu kama vile mtu mkatili angelifanya,kwa sababu hatia yako ni kubwa mnona dhambi zako ni nyingi sana.

15Kwa nini unalia kwa ajili ya jeraha lako,yale maumivu yako yasiyoponyeka?Kwa sababu ya uovu wako mkubwa na dhambi zako nyinginimekufanyia mambo haya.

16“ ‘Lakini watu wote wakuangamizao wataangamizwa;adui zako wote watakwenda uhamishoni.Wale wote wakutekao nyara watatekwa nyara;wote wakufanyao mateka nitawafanya mateka.

17Lakini nitakurudishia afya yakona kuyaponya majeraha yako,’asema Bwana,‘kwa sababu umeitwa mwenye kutupwa,Sayuni ambaye hakuna yeyote anayekujali.’

18“Hili ndilo asemalo Bwana:“ ‘Nitarudisha baraka za mahema ya Yakobo,na kuhurumia maskani yake.Mji utajengwa tena juu ya magofu yake,nalo jumba la kifalme litasimama mahali pake halisi.

19Nyimbo za kushukuru zitatoka kwaona sauti ya furaha.Nitaiongeza idadi yaowala hawatapungua,nitawapa heshimana hawatadharauliwa.

20Watoto wao watakuwa kama walivyokuwasiku za zamani,nayo jumuiya yao itaimarishwa mbele yangu;nitawaadhibu wale wote wawaoneao.

21Mmoja wao atakuwa kiongozi wao;mtawala wao atainuka miongoni mwao.Nitamleta karibu nami,naye atanikaribia mimi,kwa maana ni nani yule atakayejitoleakuwa karibu nami?’asema Bwana.

22‘Kwa hiyo ninyi mtakuwa watu wangu,nami nitakuwa Mungu wenu.’ ”

23Tazama, tufani ya Bwanaitalipuka kwa ghadhabu,upepo wa kisulisuli uendao kasiutashuka juu ya vichwa vya waovu.

24Hasira kali ya Bwana haitarudi nyumampaka atakapotimiza makusudi yote ya moyo wake.Siku zijazomtayaelewa haya.