Inapakia...
📖

Biblia Takatifu

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™
BIB 7 mistari

Yeremia 47

Yeremia • Sura 47 / 52

Ujumbe Kuhusu Wafilisti

1Hili ndilo neno la Bwana lililomjia nabii Yeremia kuhusu Wafilisti, kabla Farao hajaishambulia Gaza:

2Hili ndilo asemalo Bwana:“Tazama jinsi maji yanavyoinuka huko kaskazini,yatakuwa mafuriko yenye nguvu sana.Yataifurikia nchi na vitu vyote vilivyomo ndani yake,miji na wale waishio ndani yake.Watu watapiga kelele;wote waishio katika nchi wataomboleza

3kwa sauti ya kwato za farasi waendao mbio,kwa sauti ya magari ya adui
na mngurumo wa magurudumu yake.Baba hawatageuka kuwasaidia watoto wao,mikono yao italegea.

4Kwa maana siku imewadiakuwaangamiza Wafilisti wotena kuwakatilia mbali walionusurika woteambao wangeweza kusaidia Tiro na Sidoni.Bwana anakaribia kuwaangamiza Wafilisti,mabaki toka pwani za Kaftori.*

5Gaza atanyoa kichwa chake katika kuomboleza,Ashkeloni atanyamazishwa.Enyi mabaki kwenye tambarare,mtajikatakata wenyewe mpaka lini?

6“Mnalia, ‘Aa, upanga wa Bwana,utaendelea mpaka lini ndipo upumzike?Rudi ndani ya ala yako;acha na utulie.’

7Lakini upanga utatuliajewakati Bwana ameuamuru,wakati ameuagiza kuishambulia Ashkelonipamoja na pwani yake?”

Tanbihi

*

Kaftori ndio Krete.