1Hili ndilo neno alilosema Bwana kupitia nabii Yeremia kuhusu Babeli na nchi ya Wakaldayo:
2âTangazeni na mhubiri katikati ya mataifa,twekeni bendera na mkahubiri;
msiache kitu chochote, bali semeni,âBabeli utatekwa;Beli ataaibishwa,
Merodaki atajazwa na hofu kuu.Sanamu zake zitaaibishwana vinyago vyake vitajazwa hofu kuu.â
3Taifa kutoka kaskazini litamshambulia,na kuifanya nchi yake ukiwa.Hakuna hata mmoja atakayeishi ndani yake,watu na wanyama wataikimbia.
4âKatika siku hizo, wakati huo,âasema Bwana,âwatu wa Israeli pamoja na watu wa Yudawataenda wakilia ili kumtafuta Bwana Mungu wao.
5Wataiuliza njia iendayo Sayunina kuelekeza nyuso zao huko.Watakuja na kuambatana na Bwanakatika agano la milele
ambalo halitasahaulika.
6âWatu wangu wamekuwa kondoo waliopotea;wachungaji wao wamewapotoshana kuwasababisha kuzururajuu ya milima.Walitangatanga juu ya mlima na kilima,na kusahau mahali pao wenyewe pa kupumzikia.
7Yeyote aliyewakuta aliwala;adui zao walisema, âSisi hatuna hatia,kwa kuwa wao walitenda dhambi dhidi ya Bwana, malisho yao halisi,Bwana, aliye tumaini la baba zao.â
8âKimbieni kutoka Babeli;ondokeni katika nchi ya Wakaldayo
tena kuweni kama mbuzi wale waongozao kundi.
9Kwa maana nitaamsha na kuleta dhidi ya Babelimuungano wa mataifa makubwa kutoka nchi ya kaskazini.Watashika nafasi zao dhidi yake,naye kutokea kaskazini atatekwa.Mishale yao itakuwa kama mishale ya mashujaa walio hodari,ambao hawawezi kurudi mikono mitupu.
10Kwa hiyo Ukaldayo utatekwa nyara;wote wamtekao nyara watapata za kutosha,âasema Bwana.
11âKwa sababu hushangilia na kufurahi,wewe utekaye urithi wangu,kwa sababu unachezacheza kama mtamba anayepura nafaka,na kulia kama farasi dume,
12mama yako ataaibika mno,yeye aliyekuzaa atatahayari.Atakuwa mdogo kuliko mataifa mengine yote,atakuwa nyika, nchi kame na jangwa.
13Kwa sababu ya hasira ya Bwana hatakaliwa na mtu,lakini ataachwa ukiwa kabisa.Wote watakaopita Babeli watatiwa hofu na kudhihakikwa sababu ya majeraha yake yote.
14âShikeni nafasi zenu kuzunguka Babeli,enyi nyote mvutao upinde.Mpigeni! Msibakize mshale wowote,kwa kuwa ametenda dhambi dhidi ya Bwana.
15Piga kelele dhidi yake kila upande!Anajisalimisha, minara yake inaanguka,
kuta zake zimebomoka.Kwa kuwa hiki ni kisasi cha Bwana,mlipizeni kisasi;
mtendeeni kama alivyowatendea wengine.
16Katilieni mbali mpanzi kutoka Babeli,pamoja na mvunaji na mundu wake akivuna.Kwa sababu ya upanga wa mdhalimukila mmoja na arejee kwa watu wake mwenyewe,kila mmoja na akimbiliekwenye nchi yake mwenyewe.
17âIsraeli ni kundi lililotawanyikaambalo simba wamelifukuzia mbali.Wa kwanza kumla alikuwa mfalme wa Ashuru,wa mwisho kuponda mifupa yake
alikuwa Nebukadneza mfalme wa Babeli.â
18Kwa hiyo hili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo:âNitamwadhibu mfalme wa Babeli na nchi yakekama nilivyomwadhibu mfalme wa Ashuru.
19Lakini nitamrudisha Israeli katika malisho yake mwenyewenaye atalisha huko Karmeli na Bashani;njaa yake itashibishwajuu ya vilima vya Efraimu na Gileadi.
20Katika siku hizo, wakati huo,âasema Bwana,âuchunguzi utafanyika kwa ajili ya kosa la Israeli,lakini halitakuwepo,kwa ajili ya dhambi za Yuda,lakini haitapatikana hata moja,kwa kuwa nitawasamehemabaki nitakaowaacha.
21âShambulieni nchi ya Merathaimuna wale waishio huko Pekodi.Wafuatieni, wauenina kuwaangamiza kabisa,âasema Bwana.âFanyeni kila kitu nilichowaamuru.
22Kelele ya vita iko ndani ya nchi,kelele ya maangamizi makuu!
23Tazama jinsi nyundo ya dunia yoteilivyovunjika na kuharibika!Tazama jinsi Babeli ilivyokuwa ukiwamiongoni mwa mataifa!
24Nimetega mtego kwa ajili yako, ee Babeli,nawe ukakamatwa kabla haujafahamu;ulipatikana na ukakamatwakwa sababu ulimpinga Bwana.
25Bwana amefungua ghala lake la silahana kuzitoa silaha za ghadhabu yake,kwa kuwa Bwana Mwenyezi Mwenye Nguvu Zoteanayo kazi ya kufanya
katika nchi ya Wakaldayo.
26Njooni dhidi yake kutoka mbali.Zifungueni ghala zake za nafaka;
mlundikeni kama lundo la nafaka.Mwangamizeni kabisana msimwachie mabaki yoyote.
27Waueni mafahali wake wachanga wote;waacheni washuke machinjoni!Ole wao! Kwa kuwa siku yao imewadia,wakati wao wa kuadhibiwa.
28Wasikilizeni watoro na wakimbizi kutoka Babeliwakitangaza katika Sayunijinsi Bwana, Mungu wetu alivyolipiza kisasi,kisasi kwa ajili ya Hekalu lake.
29âWaiteni wapiga mishale dhidi ya Babeli,wote wale wavutao upinde.Pigeni kambi kumzunguka kabisa,asitoroke mtu yeyote.Mlipizeni kwa matendo yake;mtendeeni kama alivyotenda.Kwa kuwa alimdharau Bwana,yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli.
30Kwa hiyo, vijana wake wanaume wataanguka barabarani;askari wake wote watanyamazishwa siku ile,âasema Bwana.
31âTazama, niko kinyume nawe, ewe mwenye majivuno,âasema Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote,âkwa kuwa siku yako imewadia,yaani, wakati wako wa kuadhibiwa.
32Mwenye majivuno atajikwaa na kuanguka,wala hakuna yeyote atakayemuinua;nitawasha moto katika miji yake,utakaowateketeza wote wanaomzunguka.â
33Hili ndilo asemalo Bwana Mwenye Nguvu Zote:âWatu wa Israeli wameonewa,nao watu wa Yuda pia.Wote waliowateka wamewashikilia sana,wanakataa kuwaachia waende.
34Lakini Mkombozi wao ana nguvu;Bwana Mwenye Nguvu Zote ndilo jina lake.Atatetea kwa nguvu shauri laoili alete raha katika nchi yao,lakini ataleta msukosukokwa wale waishio Babeli.
35âUpanga dhidi ya Wakaldayo!âasema Bwana,âdhidi ya wale waishio Babelina dhidi ya maafisa wake na watu wenye busara!
36Upanga dhidi ya manabii wake wa uongo!Watakuwa wapumbavu.Upanga dhidi ya mashujaa wake!Watajazwa na hofu kuu
37Upanga dhidi ya farasi na magari yake ya vitapamoja na askari wake wote wa kigeni katika safu zake!
Wao watakuwa kama wanawake.Upanga dhidi ya hazina zake!Hizo zitatekwa nyara.
38Ukame juu ya maji yake!Nayo yatakauka.Kwa kuwa ni nchi ya sanamu,wao wanaenda wazimu kwa ajili ya sanamu.
39âKwa hiyo, viumbe vya jangwani na fisi wataishi humo,nao bundi watakaa humo.Kamwe haitakaliwa tenawala watu hawataishi humo kutoka kizazi hadi kizazi.
40Kama vile Mungu alivyoangamiza Sodoma na Gomorapamoja na miji iliyokuwa jirani nayo,âasema Bwana,âvivyo hivyo hakuna mtu yeyoteatakayeishi humo.Naam, hakuna mtu yeyoteatakayekaa humo.
41âTazama! Jeshi linakuja kutoka kaskazini;taifa kubwa na wafalme wengi
wanaamshwa kutoka miisho ya dunia.
42Wamejifunga pinde na mikuki;ni wakatili na wasio na huruma.Wanatoa sauti kama bahari inayongurumawanapoendesha farasi zao;wanakuja kama watu waliojipanga tayari kwa vitaili kukushambulia, ee Binti Babeli.
43Mfalme wa Babeli amesikia habari kuwahusu,nayo mikono yake imelegea.Uchungu umemshika,maumivu kama ya mwanamke katika utungu wa kuzaa.
44Kama simba anayepanda kutoka vichaka vya Yordanikuja kwenye nchi ya malisho mengi,ndivyo nitamfukuza Babeli kutoka nchi yake ghafula.Ni nani aliye mteule,
nitakayemweka kwa ajili ya jambo hili?Ni nani aliye kama mimi,na ni nani awezaye kunipinga?Tena ni mchungaji yupiawezaye kusimama kinyume nami?â
45Kwa hiyo, sikia kile Bwana alichokipanga dhidi ya Babeli,kile alichokusudia dhidi ya nchi ya Wakaldayo:Aliye mchanga katika kundi ataburutwa mbali.Yeye ataharibu kabisa malisho yao kwa sababu yao.
46Kwa sauti ya kutekwa kwa Babeli, dunia itatetemeka;kilio chake kitasikika pote miongoni mwa mataifa.