1Siku ya tatu kulikuwa na arusi katika mji wa Kana ya Galilaya, naye mama yake Yesu alikuwepo pale.
2Yesu pamoja na wanafunzi wake walikuwa wamealikwa arusini pia.
3Divai ilipokwisha, mama yake Yesu akamwambia, âWameishiwa na divai.â
4Yesu akamwambia,âMwanamke, nina nini nawe? Saa yangu haijawadia.â
5Mama yake akawaambia wale watumishi, âLolote atakalowaambia, fanyeni.â
6Basi ilikuwepo mitungi sita ya kuhifadhia maji iliyotengenezwa kwa mawe kwa ajili ya kujitakasa kwa desturi ya Kiyahudi; kila mtungi ungeweza kuchukua vipipa viwili au vitatu.*
7Yesu akawaambia wale watumishi,âIjazeni hiyo mitungi maji.âNao wakaijaza ile mitungi mpaka juu.
8Kisha akawaambia,âSasa choteni hayo maji kidogo, mpelekeeni mkuu wa meza.âHivyo wakachota, wakampelekea.
9Yule mkuu wa meza akayaonja yale maji ambayo yalikuwa yamebadilika kuwa divai. Hakujua divai hiyo ilikotoka ingawa wale watumishi waliochota yale maji wao walifahamu. Basi akamwita bwana arusi kando
10akamwambia, âWatu wote hutoa kwanza divai nzuri, kisha huleta ile divai hafifu wageni wakisha kunywa vya kutosha, lakini wewe umeiweka ile nzuri kupita zote mpaka sasa.â
11Huu, ndio uliokuwa muujiza wa kwanza Yesu aliofanya Kana ya Galilaya. Hivyo Yesu alidhihirisha utukufu wake, nao wanafunzi wake wakamwamini.
12Baada ya hayo, Yesu pamoja na mama yake, ndugu zake na wanafunzi wake, walishuka mpaka Kapernaumu, wakakaa huko siku chache.
13Ilipokaribia wakati wa Pasaka ya Wayahudi, Yesu alipanda kwenda Yerusalemu.
14Huko Hekaluni aliwakuta watu wakiuza ngĘźombe, kondoo na njiwa, nao wengine walikuwa wameketi mezani wakibadili fedha.
15Akatengeneza mjeledi kutokana na kamba, akawafukuza wote kutoka kwenye eneo la Hekalu, pamoja na kondoo na ngĘźombe. Akazipindua meza za wale wabadili fedha na kuzimwaga fedha zao.
16Akawaambia wale waliokuwa wakiuza njiwa,âWaondoeni hapa! Mnathubutuje kuifanya nyumba ya Baba yangu kuwa mahali pa biashara?â
17Wanafunzi wake wakakumbuka kuwa imeandikwa: âWivu wa nyumba yako utanila.â
18Ndipo Wayahudi wakamuuliza, âUnaweza kutuonyesha ishara gani ili kuthibitisha mamlaka uliyo nayo ya kufanya mambo haya?â
19Yesu akawajibu,âLibomoeni hili Hekalu, nami nitalijenga tena kwa siku tatu!â
20Wale Wayahudi wakamjibu, âHekalu hili lilijengwa kwa muda wa miaka arobaini na sita, nawe wasema utalijenga kwa siku tatu?â
21Lakini yeye Hekalu alilozungumzia ni mwili wake.
22Baada ya kufufuliwa kutoka kwa wafu, wanafunzi wake wakakumbuka yale aliyokuwa amesema. Ndipo wakayaamini Maandiko na yale maneno Yesu aliyokuwa amesema.
23Ikawa Yesu alipokuwa Yerusalemu kwenye Sikukuu ya Pasaka, watu wengi waliona ishara na miujiza aliyokuwa akifanya, wakaamini katika jina lake.
24Lakini Yesu hakujiaminisha kwao kwa sababu aliwajua wanadamu wote.
25Hakuhitaji ushuhuda wa mtu yeyote kuhusu mtu, kwa kuwa alijua yote yaliyokuwa moyoni mwa mtu.
Tanbihi
Kipipa kimoja chenye ujazo wa lita 40; hivyo kila mtungi ulikuwa na ujazo wa lita 80 au 120.