1Ndipo Elifazi Mtemani akajibu:
2“Kama mtu akithubutu kuzungumza nawe,kutakukasirisha?Lakini ni nani awezayekujizuia asiseme?
3Fikiri jinsi ambavyo umewafundisha watu wengi,jinsi ambavyo umeitia nguvu
mikono iliyokuwa dhaifu.
4Maneno yako yamewategemeza wale waliojikwaa;umeyatia nguvu magoti yaliyokuwa dhaifu.
5Lakini sasa hii taabu imekujia wewe,nawe unashuka moyo;imekupiga wewe,nawe unafadhaika.
6Je, kumcha Mungu kwako hakupaswi kuwandiyo matumaini yakona njia zako kutokuwa na lawamandilo taraja lako?
7“Fikiri sasa: Ni mtu yupi asiye na hatia ambaye aliwahi kuangamia?Ni wapi wanyofu waliwahi kuangamizwa?
8Kwa jinsi ambavyo mimi nimechunguza,wale walimao ubayana wale hupanda uovu,huvuna hayo hayo hayo.
9Kwa pumzi ya Mungu huangamizwa;kwa mshindo wa hasira zake huangamia.
10Simba anaweza kunguruma na kukoroma,lakini bado meno ya simba mkubwa huvunjika.
11Simba anaweza kuangamia kwa kukosa mawindo,nao wana wa simba jike hutawanyika.
12“Neno lililetwa kwangu kwa siri,masikio yangu yakasikia mnongʼono wake.
13Katikati ya ndoto za kutia wasiwasi wakati wa usiku,hapo usingizi mzito uwapatapo wanadamu,
14hofu na kutetemeka kulinishikana kufanya mifupa yangu yote itetemeke.
15Kuna roho aliyepita mbele ya uso wangu,nazo nywele za mwili wangu zikasimama.
16Yule roho akasimama,lakini sikuweza kutambua kilikuwa kitu gani.Umbo fulani lilisimama mbele ya macho yangu,kukawa na ukimya kisha nikasikia sauti:
17‘Je, binadamu aweza kuwa mwadilifu kuliko Mungu?Je, mtu aweza kuwa safi kuliko Muumba wake?
18Kama Mungu hawaamini watumishi wake,kama yeye huwalaumu malaika zake kwa kukosea,
19ni mara ngapi zaidi wale waishio katika nyumbaza udongo wa mfinyanzi,ambazo misingi yake ipo mavumbini,ambao wamepondwa kama nondo!
20Kati ya mawio na machweohuvunjwa vipande vipande;bila yeyote kutambua,huangamia milele.
21Je, kamba za hema yao hazikungʼolewa,hivyo hufa bila hekima?’