1Kisha Ayubu akajibu:
2âNaam, najua hili ni kweli.Lakini mwanadamu awezaje kuwa mwadilifu mbele za Mungu?
3Ingawa mtu angetaka kushindana naye,asingaliweza kumjibu Mungu hata mara moja miongoni mwa elfu moja.
4Hekima yake ni kubwa sana na ana uwezo mwingi mno.Ni nani aliyempinga naye akawa salama?
5Aiondoa milima bila yenyewe kujuana kuipindua kwa hasira yake.
6Aitikisa dunia kutoka mahali pakena kuzifanya nguzo zake zitetemeke.
7Husema na jua, nalo likaacha kuangaza;naye huizima mianga ya nyota.
8Yeye peke yake huzitandaza mbinguna kuyakanyaga mawimbi ya bahari.
9Yeye ndiye Muumba wa nyota za Dubu,*na Orioni,*Kilimia,*na makundi ya nyota za kusini.
10Hutenda maajabu yasiyopimika,miujiza isiyoweza kuhesabiwa.
11Anapopita karibu nami, siwezi kumwona;apitapo mbele yangu, simtambui.
12Anapochukua kwa ghafula, ni nani awezaye kumzuia?Ni nani awezaye kumwambia, âUnafanya nini?â
13Mungu hataizuia hasira yake;hata jeshi kubwa la Rahabu*lenye nguvu
linajikunyata miguuni pake.
14âNi vipi basi mimi nitaweza kubishana naye?Nawezaje kupata maneno ya kuhojiana naye?
15Ingawa sikuwa na hatia, sikuweza kumjibu;ningeweza tu kumsihi Mhukumu wangu anihurumie.
16Hata kama ningemwita kwenye shauri, naye akakubali,siamini kama angenisikiliza.
17Yeye angeniangamiza kwa dhorubana kuongeza majeraha yangu pasipo na sababu.
18Asingeniacha nipumuebali angenifunika kabisa na huzuni kuu.
19Kama ni suala la nguvu, yeye ni mwenye nguvu!Kama ni suala la haki, ni nani awezaye kumwita mahakamani?
20Hata kama sikuwa na hatia, kinywa changu kingenihukumu;kama sikuwa na kosa, kingenitangaza kuwa mwenye hatia.
21âIngawa mimi sina kosa,haileti tofauti katika nafsi yangu;
nauchukia uhai wangu.
22Hayo yote ni sawa; ndiyo sababu nasema,âYeye huwaangamiza wasio na makosa pamoja na waovu.â
23Wakati pigo liletapo kifo cha ghafula,yeye hudhihaki kule kukata tamaa kwa yule asiye na kosa.
24Wakati nchi inapoangukia mikononi mwa waovu,yeye huwafunga macho mahakimu wake.
Kama si yeye, basi ni nani?
25âSiku zangu zapita mbio kuliko mkimbiaji;zinapita upesi bila kuona furaha hata kidogo.
26Zinapita upesi kama mashua ya mafunjo,mfano wa tai ayashukiaye mawindo kwa ghafula.
27Kama nikisema, âNitayasahau malalamiko yangu,nitabadili sura ya uso wangu na kutabasamu,â
28bado ninahofia mateso yangu yote,kwa kuwa ninajua hutanihesabu kuwa sina hatia.
29Kwa kuwa nimeonekana mwenye hatia,kwa nini basi nitaabishwe bure?
30Hata kama ningejiosha kwa sabunina kutakasa mikono yangu kwa magadi,
31wewe ungenitupa kwenye shimo la utelezikiasi kwamba hata nguo zangu zingenichukia sana.
32âYeye si mwanadamu kama mimi ili niweze kumjibu,ili kwamba tuweze kushindana naye mahakamani.
33Laiti angelikuwepo mtu wa kutupatanisha kati yetu,aweke mkono wake juu yetu sote wawili,
34mtu angeliiondoa fimbo ya Mungu juu yangu,ili utisho wake usiendelee kunitia hofu.
35Ndipo ningenena naye, bila kumwogopa,lakini kama ilivyo kwangu sasa, sitaweza.
Tanbihi
Nyota za Dubu hapa ina maana ya kundi la nyota za kaskazini, ambazo zinaitwa kwa jina la Dubu Mkuu.
Orioni ni kundi la nyota kubwa.
Kilimia ni jina lililopewa nyota saba (Taurus).
Rahabu hapa ina maana ya Misri kwa fumbo.