1Akiwa ndani ya tumbo la nyangumi, Yona alimwomba Bwana Mungu wake.
2Akasema:“Katika shida yangu nalimwita Bwana,naye akanijibu.Kutoka kina cha kaburi*niliomba msaada,nawe ukasikiliza kilio changu.
3Ulinitupa kwenye kilindi,ndani kabisa ya moyo wa bahari,
mikondo ya maji ilinizunguka,mawimbi yako yote na viwimbivilipita juu yangu.
4Nikasema, ‘Nimefukuziwambali na uso wako,hata hivyo nitatazama tenakuelekea Hekalu lako takatifu.’
5Maji yaliyonimeza yalinitisha,kilindi kilinizunguka;
mwani*ulijisokota kichwani pangu.
6Nilizama chini sana mpaka pande za mwisho za milima,makomeo ya hiyo nchi yalinifungia hata milele.Lakini uliuleta uhai wangu kutoka shimoni,Ee Bwana Mungu wangu.
7“Wakati uhai wangu ulipokuwa unatoka,nilikukumbuka wewe, Bwana,nayo maombi yangu yalikufikia wewe,katika Hekalu lako takatifu.
8“Wale watu wanaongʼangʼana na sanamu zisizofaahupoteza neema ile ambayo ingekuwa yao.
9Lakini mimi, kwa wimbo wa shukrani,nitakutolea dhabihu.Lile nililowekea nadhiri nitalitimiza.Wokovu watoka kwa Bwana.”
10Basi Bwana akamwamuru yule nyangumi, naye akamtapika Yona katika nchi kavu.
Tanbihi
Kaburi hapa maana yake ni Kuzimu, kwa Kiebrania ni Sheol.
Mwani hapa maana yake ni magugu yaotayo kwenye sakafu ya kilindi cha bahari.