1Hawa ndio wafalme wa nchi ambao Waisraeli waliwashinda na kuitwaa nchi yao upande wa mashariki mwa Yordani, kuanzia Bonde la Arnoni mpaka Mlima Hermoni, pamoja na eneo lote la upande wa mashariki ya Araba:
2Sihoni mfalme wa Waamori, ambaye alitawala huko Heshboni. Alitawala kuanzia Aroeri kwenye ukingo wa Bonde la Arnoni, kuanzia katikati ya bonde, hadi kwenye Mto Yaboki, ambao ni mpaka wa Waamoni. Hii ilijumlisha nusu ya Gileadi.
3Pia alitawala Araba ya mashariki kuanzia Bahari ya Kinerethi*hadi Bahari ya Araba (yaani Bahari ya Chumvi*), hadi Beth-Yeshimothi, kisha kuelekea kusini chini ya materemko ya Pisga.
4Nayo nchi ya Ogu mfalme wa Bashani, aliyekuwa mmoja wa mabaki ya Warefai, aliyetawala Ashtarothi na Edrei.
5Naye alitawala katika Mlima Hermoni, Saleka, Bashani yote hadi mpaka wa watu wa Geshuri, na watu wa Maaka na nusu ya Gileadi, hadi kwenye mpaka wa Sihoni mfalme wa Heshboni.
6Mose, mtumishi wa Bwana, na Waisraeli wakawashinda. Naye Mose mtumishi wa Bwana akawapa Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase nchi ya hao wafalme ili iwe milki yao.
7Hawa ndio wafalme wa nchi ambao Yoshua na Waisraeli waliwashinda upande wa magharibi mwa Yordani, kuanzia Baal-Gadi katika Bonde la Lebanoni hadi kufikia Mlima Halaki, unaoinuka ukielekea Seiri. (Yoshua alitoa nchi zao kwa makabila ya Israeli iwe urithi wao sawasawa na mgawanyiko wa makabila yao:
8nchi ya vilima, shefela, upande wa magharibi, Araba, materemko ya milima, jangwa, na Negebu; nchi za Wahiti, Waamori, Wakanaani, Waperizi, Wahivi na Wayebusi):
9mfalme wa Yerikommojamfalme wa Ai (karibu na Betheli)mmoja
10mfalme wa Yerusalemummojamfalme wa Hebronimmoja
11mfalme wa Yarmuthimmojamfalme wa Lakishimmoja
12mfalme wa Eglonimmojamfalme wa Gezerimmoja
13mfalme wa Debirimmojamfalme wa Gederimmoja
14mfalme wa Hormammojamfalme wa Aradimmoja
15mfalme wa Libnammojamfalme wa Adulamummoja
16mfalme wa Makedammojamfalme wa Bethelimmoja
17mfalme wa Tapuammojamfalme wa Heferimmoja
18mfalme wa Afekimmojamfalme wa Lasharonimmoja
19mfalme wa Madonimmojamfalme wa Hazorimmoja
20mfalme wa Shimron-Meronimmojamfalme wa Akishafummoja
21mfalme wa Taanakimmojamfalme wa Megidommoja
22mfalme wa Kedeshimmojamfalme wa Yokneamu katika Karmelimmoja
23mfalme wa Dori (katika Nafoth-Dori)*mmojamfalme wa Goimu katika Gilgalimmoja
24mfalme wa Tirsammoja wafalme jumla yao ilikuwa thelathini na mmoja.
Tanbihi
Yaani Bahari ya Galilaya.
Yaani Bahari Mfu.
Au: katika miinuko ya Nafoth-Dori.