1Bwana akamwambia Mose,
2âSema na kusanyiko lote la Israeli na uwaambie: âKuweni watakatifu, kwa kuwa mimi, Bwana Mungu wenu, ni mtakatifu.
3â âKila mmoja wenu ni lazima amheshimu mama yake na baba yake, na pia ni lazima kuzishika Sabato zangu. Mimi ndimi Bwana Mungu wenu.
4â âMsiabudu sanamu, wala msijitengenezee miungu ya shaba. Mimi ndimi Bwana Mungu wenu.
5â âMnapotoa dhabihu ya sadaka ya amani kwa Bwana, toeni kwa namna ambayo itakubaliwa kwa niaba yenu.
6Sadaka hiyo italiwa siku iyo hiyo mnayoitoa, au kesho yake; chochote kitakachobaki hadi siku ya tatu lazima kiteketezwe kwa moto.
7Kama sehemu yoyote ya sadaka hiyo italiwa siku ya tatu, itakuwa si safi, nayo haitakubaliwa.
8Yeyote atakayekula atawajibishwa, kwa sababu amenajisi kitu kilicho kitakatifu kwa Bwana; mtu huyo lazima akatiliwe mbali na watu wake.
9â âWakati uvunapo mavuno ya nchi yako, usivune hadi kwenye mipaka ya shamba lako, wala usikusanye mabaki ya mavuno yako.
10Usirudi mara ya pili katika shamba lako la mizabibu, wala usiokote zabibu zilizoanguka chini. Ziache kwa ajili ya maskini na mgeni. Mimi ndimi Bwana Mungu wako.
11â âUsiibe. â âUsiseme uongo. â âMsidanganyane.
12â âUsiape kwa uongo kwa Jina langu, na hivyo kulinajisi jina la Mungu wako. Mimi ndimi Bwana.
13â âUsimdhulumu wala kumwibia jirani yako. â âUsishikilie mshahara wa kibarua usiku kucha hadi asubuhi.
14â âUsimlaani kiziwi, wala usiweke kikwazo mbele ya kipofu, lakini umche Mungu wako. Mimi ndimi Bwana.
15â âUsipotoshe haki; usionyeshe kumpendelea maskini, wala upendeleo kwa mwenye cheo, bali mwamulie jirani yako kwa haki.
16â âUsieneze uchochezi miongoni mwa watu wako. â âUsifanye kitu chochote kile kinachohatarisha maisha ya jirani yako. Mimi ndimi Bwana.
17â âUsimchukie ndugu yako moyoni mwako. Karipia jirani yako kwa uwazi ili usishiriki hatia yake.
18â âUsijilipizie kisasi wala kuwa na kinyongo dhidi ya mmoja wa jamaa yako, lakini mpende jirani yako kama unavyojipenda wewe mwenyewe. Mimi ndimi Bwana.
19â âMtazishika amri zangu. â âUsiwaache wanyama wako wa kufugwa wakazaana na wengine wa aina tofauti. â âUsipande mbegu za aina mbili katika shamba lako. â âUsivae nguo iliyofumwa kwa nyuzi za aina mbili tofauti.
20â âKama mwanaume anakutana kimwili na mwanamke ambaye ni msichana mtumwa aliyeposwa na mwanaume mwingine, lakini ambaye hajakombolewa wala hajapewa uhuru, lazima iwepo adhabu inayofaa. Hata hivyo hawatauawa, kwa sababu msichana alikuwa bado hajaachwa huru.
21Lakini huyo mtu lazima alete kondoo dume kwenye ingilio la Hema la Kukutania kwa ajili ya sadaka ya hatia kwa Bwana.
22Kupitia kwa huyo kondoo dume wa sadaka ya hatia, kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake mbele za Bwana kwa ajili ya dhambi aliyotenda, naye atasamehewa dhambi yake.
23â âMtakapoingia katika hiyo nchi na kupanda aina yoyote ya mti wa matunda, hesabuni matunda yake kama yaliyokatazwa. Kwa miaka mitatu mtayahesabu kwamba yamekatazwa; hayaruhusiwi kuliwa.
24Katika mwaka wa nne matunda yote ya mti huo yatakuwa matakatifu, sadaka ya sifa kwa Bwana.
25Bali katika mwaka wa tano mnaweza kula matunda ya mti huo. Kwa njia hii mavuno yenu yataongezewa. Mimi ndimi Bwana Mungu wako.
26â âMsile nyama yoyote yenye damu ndani yake. â âMsifanye uaguzi wala uchawi.
27â âMsikate nywele za kichwa denge, wala kunyoa pembe za ndevu zenu.
28â âMsichanje chale miili yenu kwa ajili ya mfu, wala msijichore alama juu ya miili yenu. Mimi ndimi Bwana.
29â âUsimdhalilishe binti yako kwa kumfanya kahaba, la sivyo nchi itageukia ukahaba na kujaa uovu.
30â âShika Sabato zangu na kuheshimu mahali pangu patakatifu. Mimi ndimi Bwana.
31â âMsiende kwa waaguzi, wala msitafute wapunga pepo, kwa maana watawanajisi. Mimi ndimi Bwana Mungu wako.
32â âUwapo mbele ya mzee, simama ili kuonyesha heshima kwa wazee, nawe umche Mungu wako. Mimi ndimi Bwana.
33â âWakati mgeni anaishi pamoja nawe katika nchi yako, usimnyanyase.
34Mgeni anayeishi pamoja nawe ni lazima umtendee kama mmoja wa wazawa wa nchi yako. Mpende kama unavyojipenda mwenyewe, kwa maana ulikuwa mgeni katika nchi ya Misri. Mimi ndimi Bwana Mungu wako.
35â âUsitumie vipimo vya udanganyifu unapopima urefu, kupima uzito, wala kupima wingi.
36Tumia mizani halali, mawe ya kupimia uzito halali, efa*halali, na hini*halali. Mimi ndimi Bwana Mungu wako, ambaye alikutoa katika nchi ya Misri.
37â âShika amri zangu zote na sheria zangu zote, nawe uzifuate. Mimi ndimi Bwana.â â
Tanbihi
Efa kilikuwa kipimo cha vitu vikavu.
Hini kilikuwa kipimo cha vitu vimiminika.