1Yesu akasema nao tena kwa mifano, akawaambia,
2âUfalme wa Mbinguni unaweza kufananishwa na mfalme mmoja aliyemwandalia mwanawe karamu ya arusi.
3Akawatuma watumishi wake kuwaita wale waliokuwa wamealikwa karamuni, lakini wakakataa kuja.
4âKisha akawatuma watumishi wengine akisema, âWaambieni wale walioalikwa kwamba nimeandaa chakula. Nimekwisha kuchinja mafahali wangu na vinono, karamu iko tayari. Karibuni kwa karamu ya arusi.â
5âLakini hawakuzingatia, wakaenda zao: huyu shambani mwake na mwingine kwenye biashara zake.
6Wengine wao wakawakamata wale watumishi wake, wakawatesa na kuwaua.
7Yule mfalme akakasirika sana, akapeleka jeshi lake likawaangamiza wale wauaji na kuuteketeza mji wao kwa moto.
8âKisha akawaambia watumishi wake, âKaramu ya arusi imeshakuwa tayari, lakini wale niliowaalika hawakustahili kuja.
9Kwa hiyo nendeni katika njia panda mkamwalike karamuni yeyote mtakayemwona.â
10Wale watumishi wakaenda barabarani, wakawakusanya watu wote waliowaona, wema na wabaya. Ukumbi wa arusi ukajaa wageni.
11âLakini mfalme alipoingia ndani ili kuwaona wageni, akamwona mle mtu mmoja ambaye hakuwa amevaa vazi la arusi.
12Mfalme akamuuliza, âRafiki, uliingiaje humu bila vazi la arusi?â Yule mtu hakuwa na la kusema.
13âNdipo mfalme akawaambia watumishi wake, âMfungeni mikono na miguu mkamtupe nje, kwenye giza. Huko kutakuwa na kilio na kusaga meno.â
14âKwa maana walioitwa ni wengi, lakini walioteuliwa ni wachache.â
15Ndipo Mafarisayo wakatoka nje wakaandaa mpango wa kumtega Yesu katika maneno yake.
16Wakatuma wanafunzi wao kwake pamoja na Maherode. Nao wakasema, âMwalimu, tunajua kwamba wewe ni mtu mwadilifu na unafundisha njia ya Mungu katika kweli bila kuyumbishwa na mtu wala kuonyesha upendeleo.
17Tuambie basi, wewe unaonaje? Je, ni halali kulipa kodi kwa Kaisari, au la?â
18Lakini Yesu, akijua makusudi yao mabaya, akawaambia,âEnyi wanafiki, kwa nini mnajaribu kunitega?
19Nionyesheni hiyo sarafu inayotumika kwa kulipia kodi.âWakamletea dinari.
20Naye akawauliza,âSura hii ni ya nani? Na maandishi haya ni ya nani?â
21Wakamjibu, âNi vya Kaisari.â Basi Yesu akawaambia,âMpeni Kaisari kilicho cha Kaisari, naye Mungu mpeni kilicho cha Mungu.â
22Waliposikia hili, wakashangaa. Hivyo wakamwacha, wakaenda zao.
23Siku hiyo hiyo Masadukayo, wale wasemao kwamba hakuna ufufuo wa wafu, wakamjia Yesu na kumuuliza swali, wakisema,
24âMwalimu, Mose alisema, âKama mtu akifa bila kuwa na watoto, ndugu yake inampasa amwoe huyo mjane ili ampatie watoto huyo nduguye aliyekufa.â
25Basi palikuwa na ndugu saba miongoni mwetu. Yule wa kwanza akaoa mke, naye akafa, na kwa kuwa hakuwa na watoto, akamwachia nduguye yule mjane.
26Ikatokea vivyo hivyo kwa yule ndugu wa pili, na wa tatu, hadi wote saba.
27Hatimaye, yule mwanamke naye akafa.
28Sasa basi, siku ya ufufuo, yeye atakuwa mke wa nani miongoni mwa wale ndugu saba, kwa kuwa wote walikuwa wamemwoa huyo mwanamke?â
29Yesu akawajibu,âMwapotoka kwa sababu hamjui Maandiko wala uweza wa Mungu.
30Wakati wa ufufuo, watu hawataoa wala kuolewa, bali watakuwa kama malaika wa mbinguni.
31Lakini kuhusu ufufuo wa wafu, hamjasoma kile Mungu alichowaambia, kwamba,
32âMimi ni Mungu wa Abrahamu, Mungu wa Isaki, na Mungu wa Yakoboâ? Yeye si Mungu wa wafu, bali ni Mungu wa walio hai.â
33Ule umati wa watu uliposikia hayo, ulishangaa sana kwa mafundisho yake.
34Mafarisayo waliposikia kwamba Yesu alikuwa amewanyamazisha Masadukayo, Mafarisayo wakakusanyika pamoja.
35Mmoja wao, mtaalamu wa sheria, akamuuliza swali ili kumjaribu, akisema,
36âMwalimu, ni amri ipi katika Sheria iliyo kuu kuliko zote?â
37Yesu akamjibu,â âMpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote na kwa akili zako zote.â
38Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza.
39Nayo ya pili ni kama hiyo, nayo ni hii: âMpende jirani yako kama nafsi yako.â
40Amri hizi mbili ndizo msingi wa Sheria na Manabii.â
41Wakati Mafarisayo walikuwa wamekusanyika pamoja, Yesu akawauliza,
42âMnaonaje kuhusu Kristo?*Yeye ni mwana wa nani?âWakamjibu, âYeye ni mwana wa Daudi.â
43Akawaambia,âInakuwaje basi kwamba Daudi, akinena kwa kuongozwa na Roho, anamwita Kristo âBwanaâ? Kwa maana asema,
44â âBwana alimwambia Bwana wangu:âKeti mkono wangu wa kuume,hadi nitakapowaweka adui zakochini ya miguu yako.â â
45Kama basi Daudi anamwita yeye âBwana,â awezaje kuwa mwanawe?â
46Hakuna mtu aliyeweza kumjibu Yesu neno. Tena tangu siku hiyo hakuna aliyethubutu kumuuliza tena maswali.
Tanbihi
Kristo maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta.