1Yesu aliposhuka kutoka mlimani, makutano makubwa ya watu yakamfuata.
2Mtu mmoja mwenye ukoma akaja na kupiga magoti mbele yake, akasema, âBwana, kama ukitaka, unaweza kunitakasa.â
3Yesu akanyoosha mkono wake akamgusa yule mtu, akamwambia,âNataka. Takasika!âMara yule mtu akatakasika ukoma wake.
4Kisha Yesu akamwambia,âHakikisha humwambii mtu yeyote. Lakini nenda ukajionyeshe kwa kuhani, na utoe sadaka aliyoamuru Mose, ili kuwa ushuhuda kwao.â
5Yesu alipoingia Kapernaumu, jemadari mmoja alimjia, kumwomba msaada,
6akisema, âBwana, mtumishi wangu amelala nyumbani na amepooza, tena ana maumivu makali ya kutisha.â
7Yesu akamwambia,âNitakuja na kumponya.â
8Lakini yule jemadari akamwambia, âBwana, mimi sistahili wewe kuingia chini ya dari yangu. Lakini sema neno tu, naye mtumishi wangu atapona.
9Kwa kuwa mimi mwenyewe ni mtu niliyewekwa chini ya mamlaka, nikiwa na askari chini yangu. Nikimwambia huyu, âNenda,â yeye huenda; na mwingine nikimwambia, âNjoo,â yeye huja. Nikimwambia mtumishi wangu, âFanya hivi,â yeye hufanya.â
10Yesu aliposikia maneno haya, alishangaa, akawaambia wale waliomfuata,âAmin, nawaambia, hata katika Israeli sijapata kuona yeyote mwenye imani kubwa namna hii.
11Ninawaambia kwamba wengi watatoka mashariki na magharibi, nao wataketi karamuni pamoja na Abrahamu, Isaki na Yakobo katika Ufalme wa Mbinguni.
12Lakini warithi wa Ufalme watatupwa katika giza la nje, ambako kutakuwako kilio na kusaga meno.â
13Kisha Yesu akamwambia yule jemadari,âNenda na iwe kwako sawasawa na imani yako.âNaye yule mtumishi akapona saa ile ile.
14Yesu alipoingia nyumbani kwa Petro, alimkuta mama mkwe wa Petro amelala kitandani, akiwa ana homa.
15Akamgusa mkono wake na homa ikamwacha, naye akainuka na kuanza kumhudumia.
16Jioni ile, wakamletea watu wengi waliopagawa na pepo wachafu, naye akawatoa wale pepo wachafu kwa neno lake, na kuwaponya wagonjwa wote.
17Haya yalifanyika ili litimie lile lililonenwa kwa kinywa cha nabii Isaya kwamba:âMwenyewe alitwaa udhaifu wetuna alichukua magonjwa yetu.â
18Yesu alipoona makutano mengi wamemzunguka, aliwaamuru wanafunzi wake wavuke mpaka ngĘźambo ya ziwa.
19Kisha mwalimu mmoja wa sheria akamjia Yesu na kumwambia, âMwalimu, nitakufuata kokote uendako.â
20Naye Yesu akamjibu,âMbweha wana mapango, nao ndege wa angani wana viota, lakini Mwana wa Adamu hana mahali pa kulaza kichwa chake.â
21Mwanafunzi mwingine akamwambia, âBwana, niruhusu kwanza nikamzike baba yangu.â
22Lakini Yesu akamwambia,âNifuate, uwaache wafu wawazike wafu wao.â
23Naye alipoingia kwenye mashua, wanafunzi wake wakamfuata.
24Ghafula, kukainuka dhoruba kali baharini hata mashua ikaanza kufunikwa na mawimbi, lakini Yesu alikuwa amelala usingizi.
25Wanafunzi wake wakamwendea na kumwamsha, wakisema, âBwana, tuokoe! Tunazama!â
26Naye Yesu akawaambia,âKwa nini mnaogopa, enyi wa imani haba?âKisha akaamka na kukemea dhoruba na mawimbi, nako kukawa shwari kabisa.
27Wale watu wakashangaa, wakisema, âNi mtu wa namna gani huyu? Hata upepo na mawimbi vinamtii!â
28Walipofika ngĘźambo katika nchi ya Wagerasi, watu wawili waliopagawa na pepo wachafu walitoka makaburini nao wakakutana naye. Watu hawa walikuwa wakali mno kiasi kwamba hakuna mtu aliyeweza kupita njia ile.
29Wakapiga kelele, âUna nini nasi, Mwana wa Mungu? Umekuja hapa kututesa kabla ya wakati ulioamriwa?â
30Mbali kidogo kutoka pale walipokuwa, kulikuwa na kundi kubwa la nguruwe wakilisha.
31Wale pepo wachafu wakamsihi Yesu, âUkitutoa humu, turuhusu twende kwenye lile kundi la nguruwe.â
32Akawaambia,âNendeni!âHivyo wakatoka na kuwaingia wale nguruwe, nalo kundi lote likateremka gengeni kwa kasi, likaingia katika ziwa na kufa ndani ya maji.
33Wale watu waliokuwa wakiwachunga hao nguruwe wakakimbia wakaingia mjini, wakaeleza yote kuhusu yale yaliyowatokea wale waliokuwa wamepagawa na pepo wachafu.
34Kisha watu wote wa mji huo wakatoka kwenda kukutana na Yesu. Nao walipomwona wakamsihi aondoke kwenye nchi yao.