1Basi Balaamu alipoona imempendeza Bwana kubariki Israeli, hakuendelea tena kutafuta uchawi kama nyakati nyingine, bali aligeuza uso wake kuelekea nyikani.
2Balaamu alipotazama nje na kuona Israeli amepiga kambi kabila kwa kabila, Roho wa Mungu akawa juu yake,
3naye akatoa ujumbe wake:âUjumbe wa Balaamu mwana wa Beori,ujumbe wake yeye ambaye jicho lake linaona vizuri;
4ujumbe wake yeye ambaye husikia maneno ya Mungu,ambaye huona maono kutoka kwa Mwenyezi,*
ambaye huanguka kifudifudi, na ambaye macho yake yamefunguka:
5âTazama jinsi yalivyo mazuri mahema yako, ee Yakobo,maskani yako, ee Israeli!
6âKama mabonde, yanaenea,kama bustani kando ya mto,kama miti ya udi iliyopandwa na Bwana,kama mierezi kando ya maji.
7Maji yatatiririka kutoka ndoo zake;mbegu yake itakuwa na maji tele.
âMfalme wake atakuwa mkuu kuliko Mfalme Agagi;ufalme wake utatukuka.
8âMungu alimleta kutoka Misri;yeye ana nguvu kama nyati.Anayararua mataifa yaliyo adui zake,na kuvunja mifupa yao vipande vipande;
huwachoma kwa mishale yake.
9Hujikunyata na kuvizia kama simba,kama simba jike; nani anayethubutu kumwamsha?
âAbarikiwe kila akubarikiye,na alaaniwe kila akulaaniye!â
10Ndipo hasira ya Balaki ikawaka dhidi ya Balaamu. Akapiga mikono yake pamoja, akamwambia Balaamu, âNilikuita uje kuwalaani adui zangu, lakini umewabariki mara hizi tatu.
11Sasa ondoka upesi uende nyumbani! Mimi nilisema nitakuzawadia vizuri sana, lakini Bwana amekuzuia usizawadiwe.â
12Balaamu akamwambia Balaki, âJe, hukumbuki jinsi nilivyowaambia wajumbe uliowatuma kwangu? Niliwaambia hivi,
13âHata ikiwa Balaki angenipa jumba lake la kifalme likiwa limejazwa fedha na dhahabu, nisingeweza kufanya kitu chochote kwa matakwa yangu, kikiwa kizuri au kibaya, kwenda kinyume na agizo la Bwana, nami imenipasa kusema tu kile Bwana atakachosemaâ?
14Sasa ninarudi kwa watu wangu. Lakini njoo, nikuonye kuhusu kile watu hawa watakachowatenda watu wako siku zijazo.â
15Kisha Balaamu akatoa ujumbe wake:âUjumbe wa Balaamu mwana wa Beori,ujumbe wake yeye ambaye jicho lake linaona vizuri;
16ujumbe wake yeye ambaye husikia maneno ya Mungu,ambaye ana maarifa kutoka kwa Aliye Juu Sana,huona maono kutoka Mwenyezi,ambaye huanguka kifudifudi
na ambaye macho yake yamefunguka:
17âNamwona yeye, lakini si sasa;namtazama yeye, lakini si karibu.Nyota itatoka kwa Yakobo,fimbo ya ufalme itainuka kutoka kwa Israeli.Atawaponda Wamoabu vipaji vya nyusona mafuvu yote ya wana wa Shethi.
18Edomu itamilikiwa,Seiri, adui wake, itamilikiwa,
lakini Israeli atakuwa na nguvu.
19Mtawala atakuja kutoka kwa Yakobona kuangamiza walionusurika katika mji.â
20Kisha Balaamu akawaona watu wa Amaleki, na kutoa ujumbe wake:âAmaleki ilikuwa ya kwanza miongoni mwa mataifa,lakini mwisho wake itaangamizwa milele.â
21Kisha akawaona Wakeni, akatoa ujumbe wake:âMakao yenu ni salama,kiota chenu kiko kwenye mwamba.
22Hata hivyo ninyi Wakeni mtaangamizwaAshuru atakapowachukua mateka.â
23Ndipo akatoa ujumbe wake:âLo, ni nani atakayeweza kuishi wakati Mungu atakapofanya hili?
24Meli zitakuja kutoka pwani za Kitimu,zitaitiisha Ashuru na Eberi,lakini nao pia wataangamizwa.â
25Kisha Balaamu akainuka na kurudi nyumbani kwake, naye Balaki akashika njia yake.
Tanbihi
Mwenyezi hapa ina maana ya Shaddai kwa Kiebrania (pia 24:16).