1Mtu ajitengaye na wenginehufuata matakwa yake mwenyewe;
hupiga vita kila shauri jema.
2Mpumbavu hafurahii ufahamu,bali hufurahia kutangaza
maoni yake mwenyewe.
3Wakati uovu unapokuja, dharau huja pia,pamoja na aibu huja lawama.
4Maneno ya kinywa cha mwanadamu ni kina cha maji,bali chemchemi ya hekima ni kijito kinachobubujika.
5Sio vizuri kumpendelea mtu mwovu,au kumnyima haki asiye na hatia.
6Midomo ya mpumbavu humletea ugomvina kinywa chake hualika kipigo.
7Kinywa cha mpumbavu ni uharibifu wakena midomo yake ni mtego kwa nafsi yake.
8Maneno ya mchongezi ni kama chakula kitamu;huingia sehemu za ndani sana za mtu.
9Mtu aliye mlegevu katika kazi yakeni ndugu na yule anayeharibu.
10Jina la Bwana ni ngome imara,wenye haki huikimbilia na kuwa salama.
11Mali ya tajiri ni mji wake wenye ngome,wanaudhania kuwa ukuta usioweza kurukwa.
12Kabla ya anguko moyo wa mtu hujaa kiburi,bali unyenyekevu hutangulia heshima.
13Yeye ajibuye kabla ya kusikiliza,huo ni upumbavu wake na aibu yake.
14Roho ya mtu itastahimili katika ugonjwabali roho iliyovunjika ni nani awezaye kuistahimili?
15Moyo wa mwenye ufahamu hujipatia maarifa,masikio ya mwenye hekima huyatafuta maarifa.
16Zawadi humfungulia njia mtoaji,nayo humleta mbele ya wakuu.
17Yeye aliye wa kwanza kuleta mashtaka huonekana sahihi,hadi mwingine ajitokezapo na kumuuliza maswali.
18Kupiga kura hukomesha mashindanona kutenganisha wapinzani wakuu wanaopingana.
19Ndugu aliyechukizwa ni mgumu kuridhikakuliko mji uliozungushiwa ngome,nayo mabishano ni kama malangoya ngome yenye makomeo.
20Tumbo la mtu litajaa kutokana na tunda la kinywa chake,atashibishwa mavuno yanayotokana na midomo yake.
21Mauti na uzima viko katika uwezo wa ulimi,nao waupendao watakula matunda yake.
22Apataye mke apata kitu chemanaye ajipatia kibali kwa Bwana.
23Mtu maskini huomba kuhurumiwabali tajiri hujibu kwa ukali.
24Mtu mwenye marafiki wengi wanaweza kumharibu,bali yuko rafiki aambatanaye na mtu kwa karibu kuliko ndugu.