Inapakia...
📖

Biblia Takatifu

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™
BIB 22 mistari

Mithali 2

Mithali • Sura 2 / 31

Faida Za Hekima

1Mwanangu, kama utayakubali maneno yanguna kuyaweka akiba maagizo yangu ndani mwako,

2kutega sikio lako kwenye hekimana kuweka moyo wako katika ufahamu,

3na kama ukiita busarana kuita kwa sauti ufahamu,

4na kama utaitafuta kama fedhana kuitafuta sana kama hazina iliyofichwa,

5ndipo utakapoelewa kumcha Bwanana kupata maarifa ya Mungu.

6Kwa maana Bwana hutoa hekima,na kinywani mwake hutoka maarifa na ufahamu.

7Anahifadhi ushindi kwa ajili ya mwadilifu,yeye ni ngao kwa wale wasio na lawama,

8kwa kuwa hulinda mwenendo wa mwenye hakina kuhifadhi njia ya waaminifu wake.

9Ndipo utafahamu lipi lililo kweli na hakina sawa: yaani kila njia nzuri.

10Kwa maana hekima itaingia moyoni mwako,nayo maarifa yataifurahisha nafsi yako.

11Busara itakuhifadhina ufahamu utakulinda.

12Hekima itakuokoa kutoka njia za waovu,kutoka kwa watu ambao maneno yao yamepotoka,

13wale waachao mapito yaliyonyookawakatembea katika njia za giza,

14wale wapendao kutenda mabayana kufurahia upotovu wa ubaya,

15ambao mapito yao yamepotokana ambao ni wapotovu katika njia zao.

16Itakuokoa pia kutokana na mwanamke kahaba,kutokana na mke aliyepotoka mwenye maneno
ya kushawishi kutenda ubaya,

17aliyemwacha mwenzi wa ujana wakena kupuuza agano alilofanya mbele ya Mungu.

18Kwa maana nyumba yake huelekea kwenye kifona mapito yake kwenye roho za waliokufa.

19Hakuna yeyote aendaye kwake akarudi,au kufikia mapito ya uzima.

20Hivyo utatembea katika njia za watu wemana kushikamana na mapito ya wenye haki.

21Kwa maana wanyofu wataishi katika nchi,nao wasio na lawama watabakia ndani yake.

22Bali waovu watakatiliwa mbali kutoka nchi,nao wasio waaminifu watangʼolewa kutoka humo.