Inapakia...
📖

Biblia Takatifu

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™
BIB 27 mistari

Mithali 27

Mithali • Sura 27 / 31

1Usijisifu kwa ajili ya kesho,kwa kuwa hujui ni nini kitakachozaliwa kwa siku moja.

2Mwache mwingine akusifu,wala si kinywa chako mwenyewe;mtu mwingine afanye hivyona si midomo yako mwenyewe.

3Jiwe ni zito na mchanga ni mzigo,lakini kukasirishwa na mpumbavu ni kuzito kuliko vyote viwili.

4Hasira ni ukatili na ghadhabu kali ni gharika,lakini ni nani awezaye kusimama mbele ya wivu?

5Afadhali karipio la wazikuliko upendo uliofichika.

6Majeraha kutoka kwa rafiki yaonyesha uaminifu,bali kubusu kwa adui ni kwingi sana.

7Yeye aliyeshiba huchukia kabisa asali,bali kwa mwenye njaa
hata kile kilicho kichungu
kwake ni kitamu.

8Kama ndege atangatangavyo mbali na kiota chake,ndivyo alivyo mtu atangatangaye
mbali na nyumbani mwake.

9Manukato na uvumba huleta furaha moyoni,nao uzuri wa rafiki huchipuka
kutoka kwenye ushauri wake wa uaminifu.

10Usimwache rafiki yako wala rafiki wa baba yako,tena usiende nyumbani mwa ndugu yako
wakati umepatwa na maafa.Bora jirani wa karibukuliko ndugu aliye mbali.

11Mwanangu, uwe na hekima,nawe ulete furaha moyoni mwangu,ndipo nitakapoweza kumjibu yeyoteanitendaye kwa dharau.

12Mtu mwenye busara huona hatari na kujificha,bali mjinga huendelea mbele nayo ikamtesa.

13Chukua vazi la yule awekaye dhamanakwa ajili ya mgeni;lishikilie iwe dhamana kama anafanya hivyokwa ajili ya mwanamke mpotovu.

14Kama mtu akimbariki jirani yake kwa sauti kuuasubuhi na mapema,
itahesabiwa kama ni laana.

15Mke mgomvi ni kamamatone yasiyokoma ya siku ya mvua.

16Kumzuia yeye ni kama kuuzuia upepoau kukamata mafuta kwa kiganja cha mkono.

17Kama vile chuma kinoavyo chuma,ndivyo mtu amnoavyo mwenzake.

18Yeye autunzaye mtini atakula tunda lake,naye amtunzaye bwana wake ataheshimiwa.

19Kama uso uonekanavyo kwenye maji,ndivyo hivyo moyo wa mtu humwonyesha alivyo.

20Kuzimu na Uharibifu havishibikadhalika macho ya mwanadamu.

21Kalibu ni kwa ajili ya fedhana tanuru kwa ajili ya dhahabu,
bali mtu hupimwa kwa sifa azipokeazo.

22Hata ukimtwanga mpumbavu kwenye kinu,ukimtwanga kama nafaka kwa mchi,
hutauondoa upumbavu wake.

23Hakikisha kuwa unajua hali ya makundi yakoya kondoo na mbuzi,
angalia kwa bidii ngʼombe zako.

24Kwa kuwa utajiri haudumu milele,nayo taji haidumu vizazi vyote.

25Wakati majani makavu yameondolewana mapya yamechipua,
nayo majani toka milimani yamekusanywa,

26wana-kondoo watakupatia mavazina mbuzi thamani ya shamba.

27Utakuwa na maziwa mengi ya mbuzikukulisha wewe na jamaa yako,
na kuwalisha watumishi wako wa kike.