Inapakia...
📖

Biblia Takatifu

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™
BIB 23 mistari

Mithali 5

Mithali • Sura 5 / 31

Onyo Dhidi Ya Uzinzi

1Mwanangu, sikiliza kwa makini hekima yangu,sikiliza vizuri maneno yangu ya busara,

2ili uweze kutunza busarana midomo yako ihifadhi maarifa.

3Kwa maana midomo ya mwanamke kahabahudondoza asali,na maneno ya kinywa chakeni laini kuliko mafuta;

4lakini mwisho wake ni mchungu kama nyongo,mkali kama upanga ukatao kuwili.

5Miguu yake hushuka kuelekea kwenye kifo;hatua zake huelekea moja kwa moja kaburini.*

6Yeye hafikiri juu ya njia ya uzima;njia zake zimepotoka, lakini yeye hajui.

7Sasa basi wanangu, nisikilizeni;msiache ninalowaambia.

8Njia zenu ziwe mbali naye,msiende karibu na mlango wa nyumba yake,

9usije ukatoa nguvu zako nzuri kwa wenginena miaka yako kwa aliye mkatili,

10wageni wasije wakasherehekea utajiri wakona jitihada yako ikatajirisha
nyumba ya mwanaume mwingine.

11Mwishoni mwa maisha yako utalia kwa uchungu,wakati nyama na mwili wako vimechakaa.

12Utasema, “Tazama jinsi gani nilivyochukia adhabu!Tazama jinsi moyo wangu ulivyodharau maonyo!

13Sikuwatii walimu wanguwala kuwasikiliza wakufunzi wangu.

14Nimefika ukingoni mwa maangamizi kabisakatikati ya kusanyiko lote.”

15Kunywa maji kutoka kwenye kisima chako mwenyewe,maji yanayotiririka kutoka kwenye kisima chako mwenyewe.

16Je, chemchemi zako zifurike katika barabara za mjina vijito vyako vya maji viwanjani?

17Na viwe vyako mwenyewe,kamwe visishirikishwe wageni.

18Chemchemi yako na ibarikiwena umfurahie mke wa ujana wako.

19Kulungu jike apendaye, kulungu mzuri:matiti yake na yakutosheleze siku zote,
nawe utekwe daima na upendo wake.

20Kwa nini mwanangu, utekwe na mwanamke kahaba?Kwa nini ukumbatie kifua cha mke wa mwanaume mwingine?

21Kwa maana njia za mtu ni wazi kabisa mbele za Bwana,naye huyapima mapito yake yote.

22Matendo mabaya ya mtu mwovu humnasa yeye mwenyewe;kamba za dhambi yake humkamata kwa nguvu.

23Atakufa kwa kukosa nidhamu,akipotoshwa kwa upumbavu wake mwenyewe.

Tanbihi

*

Kaburini hapa maana yake ni Kuzimu, kwa Kiebrania ni Sheol.