1Hekima amejenga nyumba yake;amechonga nguzo zake saba.
2Ameandaa nyama na kuchanganya divai yake;pia ameandaa meza yake.
3Amewatuma watumishi wake wa kike, naye huitakutoka mahali pa juu sana pa mji.
4Anawaambia wale wasio na akili,âWote ambao ni wajinga na waje hapa!
5Njooni, mle chakula changuna mnywe divai niliyoichanganya.
6Acheni njia zenu za ujinga nanyi mtaishi;tembeeni katika njia ya ufahamu.
7âYeyote anayemkosoa mwenye mzahahukaribisha matukano;yeyote anayekemea mtu mwovuhupatwa na matusi.
8Usimkemee mwenye mzaha la sivyo atakuchukia;mkemee mwenye hekima naye atakupenda.
9Mfundishe mtu mwenye hekimanaye atakuwa na hekima zaidi;mfundishe mtu mwadilifunaye atazidi kufundishika.
10âKumcha Bwana ndicho chanzo cha hekima,na kumjua Aliye Mtakatifu ni ufahamu.
11Kwa maana kwa msaada wangusiku zako zitakuwa nyingi,
na miaka itaongezwa katika maisha yako.
12Kama wewe una hekima, hekima yako itakupa tuzo;kama wewe ni mtu wa mzaha,
wewe mwenyewe ndiwe utateseka.â
13Mwanamke aitwaye Mpumbavu ana kelele;hana adabu na hana maarifa.
14Huketi kwenye mlango wa nyumba yake,juu ya kiti katika mahali pa juu sana pa mji,
15akiita wale wapitao karibu,waendao moja kwa moja kwenye njia yao.
16Anawaambia wale wasio na akili,âWote ambao ni wajinga na waje hapa ndani!â
17âMaji yaliyoibiwa ni matamu;chakula kinacholiwa sirini ni kitamu!â
18Lakini hawajui hata kidogo kuwa wafu wako humo,kwamba wageni wake huyo mwanamke
wako katika vilindi vya kuzimu.