1Nitaimba juu ya upendo wako na haki yako;kwako wewe, Ee Bwana, nitaimba sifa.
2Nitazingatia kuishi maisha yasiyo na lawama:utakuja kwangu lini?
Nitatembea nyumbani mwangukwa moyo usio na lawama.
3Sitaweka mbele ya macho yangukitu kiovu.
Ninayachukia matendo ya watu wasio na imani;hawatashikamana nami.
4Moyo wa ukaidi utakuwa mbali nami;nitajitenga na kila ubaya.
5Kila amsingiziaye jirani yake kwa siri,huyo nitamnyamazisha;mwenye macho ya dharau na moyo wa kiburihuyo sitamvumilia.
6Macho yangu yatawaelekea waaminifu katika nchi,ili waweze kuishi pamoja nami;yeye ambaye moyo wake hauna lawamaatanitumikia.
7Mdanganyifu hatakaanyumbani mwangu,yeye asemaye kwa uongohatasimama mbele yangu.
8Kila asubuhi nitawanyamazishawaovu wote katika nchi;nitamkatilia mbali kila mtenda mabayakutoka mji wa Bwana.