1Bwana amwambia Bwana wangu:“Keti mkono wangu wa kuume,mpaka nitakapowafanya adui zakokuwa mahali pa kuweka miguu yako.”
2Bwana ataeneza fimbo yako ya utawala yenye nguvu kutoka Sayuni;utatawala katikati ya adui zako.
3Askari wako watajitolea kwa hiarikatika siku yako ya vita.Ukiwa umevikwa fahari takatifu,kutoka tumbo la mapambazuko
utapokea umande wa ujana wako.*
4Bwana ameapa,naye hatabadilisha mawazo yake:
“Wewe ni kuhani milele,
kwa mfano wa Melkizedeki.”
5Bwana yuko mkono wako wa kuume,atawaponda wafalme siku ya ghadhabu yake.
6Atawahukumu mataifa, akilundika mizogana kuwaponda watawala wa dunia nzima.
7Atakunywa maji katika kijito kando ya njia,*kwa hiyo atainua kichwa chake juu.
Tanbihi
Au: vijana wako watakujia kama umande.
Au: Yeye atoaye mtu wa kurithi mwingine atamweka kwenye mamlaka.