1Bwana tusaidie, kwa kuwa wacha Mungu wametoweka;waaminifu wametoweka miongoni mwa wanadamu.
2Kila mmoja humwambia jirani yake uongo;midomo yao ya hila huzungumza kwa udanganyifu.
3Bwana na akatilie mbali midomo yote ya hilana kila ulimi uliojaa majivuno,
4ule unaosema, “Kwa ndimi zetu tutashinda;midomo ni mali yetu, bwana wetu ni nani?”
5“Kwa sababu ya uonevu wa wanyongena kulia kwa uchungu kwa wahitaji,nitainuka sasa,” asema Bwana.“Nitawalinda kutokana na wale
wenye nia mbaya juu yao.”
6Maneno ya Bwana ni safi,kama fedha iliyosafishwa katika tanuru,
iliyosafishwa mara saba.
7Ee Bwana, utatuweka salamana kutulinda na kizazi hiki milele.
8Watu waovu huenda wakiringa kila mahaliwakati ambapo yule aliye mbaya sana
ndiye anayeheshimiwa miongoni mwa watu.