Inapakia...
📖

Biblia Takatifu

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™
BIB 9 mistari

Zaburi 122

Zaburi • Sura 122 / 150

Sifa Kwa Yerusalemu
Wimbo wa kwenda juu. Wa Daudi.

1Nilishangilia pamoja na wale walioniambia,“Twende nyumbani ya Bwana.”

2Ee Yerusalemu, miguu yetu imesimamamalangoni mwako.

3Yerusalemu imejengwa vyema kama mjiambao umeshikamanishwa pamoja.

4Huko ndiko makabila hukwea,makabila ya Bwana,kulisifu jina la Bwana kulingana na maagizowaliopewa Israeli.

5Huko viti vya enzi vya hukumu hukaa,viti vya enzi vya nyumba ya Daudi.

6Omba kwa ajili ya amani ya Yerusalemu:“Wote wakupendao na wawe salama.

7Amani na iwepo ndani ya kuta zakona usalama ndani ya ngome zako.”

8Kwa ajili ya ndugu zangu na marafiki,nitasema, “Amani iwe ndani yako.”

9Kwa ajili ya nyumba ya Bwana Mungu wetu,nitatafuta mafanikio yako.