Inapakia...
📖

Biblia Takatifu

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™
BIB 3 mistari

Zaburi 133

Zaburi • Sura 133 / 150

Sifa Za Pendo La Undugu
Wimbo wa kwenda juu. Wa Daudi.

1Tazama jinsi ilivyo vyema na kupendezawakati ndugu wanapoishi pamoja katika umoja!

2Ni kama mafuta ya thamani yaliyomiminwa kichwani,yakitiririka kwenye ndevu,yakitiririka kwenye ndevu za Aroni,mpaka kwenye upindo wa mavazi yake.

3Ni kama vile umande wa Hermoniunavyoanguka juu ya Mlima Sayuni.Kwa maana huko ndiko Bwana alikoamuru baraka yake,naam, hata uzima milele.