1Kando ya mito ya Babeli tuliketi, tukaombolezatulipokumbuka Sayuni.
2Kwenye miti ya hukotulitundika vinubi vyetu,
3kwa maana huko hao waliotutekawalitaka tuwaimbie nyimbo,watesi wetu walidai nyimbo za furaha;walisema, āTuimbieni wimbo mmoja kati ya nyimbo za Sayuni!ā
4Tutaimbaje nyimbo za Bwana,tukiwa nchi ya kigeni?
5Nikikusahau wewe, ee Yerusalemu,basi mkono wangu wa kuume na usahau ujuzi wake.
6Ulimi wangu ushikamane na kaakaa la kinywa changukama sitakukumbuka wewe,kama nisipokufikiri Yerusalemukuwa furaha yangu kubwa.
7Kumbuka, Ee Bwana, walichokifanya Waedomu,siku ile Yerusalemu ilipoanguka.Walisema, āBomoa, Bomoampaka kwenye misingi yake!ā
8Ee binti Babeli, uliyehukumiwa kuangamizwa,heri yeye atakayekulipiza wewe
kwa yale uliyotutenda sisi:
9yeye ambaye atawakamata watoto wako wachangana kuwaponda juu ya miamba.