Inapakia...
📖

Biblia Takatifu

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™
BIB • 12 mistari

Zaburi 2

Zaburi • Sura 2 / 150

Mfalme Aliyechaguliwa Na Mungu

1Kwa nini mataifa wanashauriana kufanya mabaya,na kabila za watu kula njama bure?

2Wafalme wa dunia wanajipangana watawala wanajikusanya pamojadhidi ya Bwanana dhidi ya Mpakwa Mafuta wake.

3Wanasema, “Tuvunje minyororo yaona kuvitupilia mbali vifungo vyao.”

4Yeye atawalaye mbinguni hucheka,Bwana huwadharau.

5Kisha huwakemea katika hasira yakena kuwaogopesha katika ghadhabu yake, akisema,

6“Nimemtawaza Mfalme wangujuu ya Sayuni, mlima wangu mtakatifu.”

Ushindi Wa Mfalme

7Nitatangaza amri ya Bwana:Yeye aliniambia, “Wewe ni Mwanangu,
leo mimi nimekuzaa.

8Niombe, nami nitayafanya mataifakuwa urithi wako,
miisho ya dunia kuwa milki yako.

9Utawatawala kwa fimbo ya chumana kuwavunjavunja kama chombo cha mfinyanzi.”

10Kwa hiyo, ninyi wafalme, kuweni na hekima;mwonyeke, enyi watawala wa dunia.

11Mtumikieni Bwana kwa hofuna mshangilie kwa kutetemeka.

12Mbusu Mwana, asije akakasirikanawe ukaangamizwa katika njia yako,kwa maana hasira yake inaweza kuwaka ghafula.Heri wote wanaomkimbilia.