1Bwana na akujibu unapokuwa katika dhiki,jina la Mungu wa Yakobo na liwe kinga yako.
2Na akutumie msaada kutoka patakatifuna akupatie msaada kutoka Sayuni.
3Na azikumbuke dhabihu zako zote,na azikubali sadaka zako za kuteketezwa.
4Na akujalie haja ya moyo wako,na aifanikishe mipango yako yote.
5Tutashangilia kwa furaha utakaposhinda,tutainua bendera zetu kwa jina la Mungu wetu.Bwana na akupe haja zako zote.
6Sasa nafahamu kuwa Bwanahumwokoa mpakwa mafuta wake,humjibu kutoka mbingu yake takatifukwa nguvu za wokovu wa mkono wake wa kuume.
7Wengine wanatumaini magari ya vita, na wengine farasi,bali sisi tutalitumainia jina la Bwana, Mungu wetu.
8Wao wameshushwa chini na kuanguka,bali sisi tunainuka na kusimama imara.
9Ee Bwana, mwokoe mfalme!Tujibu tunapokuita!