Inapakia...
📖

Biblia Takatifu

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™
BIB 6 mistari

Zaburi 23

Zaburi • Sura 23 / 150

Bwana Mchungaji Wetu
Zaburi ya Daudi.

1Bwana ndiye mchungaji wangu,sitapungukiwa na kitu.

2Hunilaza katika malishoya majani mabichi,kando ya maji matulivu huniongoza,

3hunihuisha nafsi yangu.Huniongoza katika njia za hakikwa ajili ya jina lake.

4Hata kama nikipita katikatiya bonde la uvuli wa mauti,sitaogopa mabaya,kwa maana wewe upo pamoja nami;fimbo yako na mkongojo wakovyanifariji.

5Waandaa meza mbele yangumachoni pa adui zangu.Umenipaka mafuta kichwani pangu,kikombe changu kinafurika.

6Hakika wema na upendo vitanifuatasiku zote za maisha yangu,nami nitakaa nyumbani mwa Bwanamilele.