Inapakia...
📖

Biblia Takatifu

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™
BIB 11 mistari

Zaburi 32

Zaburi • Sura 32 / 150

Furaha Ya Msamaha
Zaburi ya Daudi. Funzo.

1Heri mtu yule ambaye amesamehewa makosa yake,ambaye dhambi zake zimefunikwa.

2Heri mtu yule ambaye Bwanahamhesabii dhambi,na ambaye rohoni mwakehamna udanganyifu.

3Niliponyamaza, mifupa yangu ilichakaakwa kulia kwa maumivu makali mchana kutwa.

4Usiku na mchanamkono wako ulinilemea,nguvu zangu zilinyonywakama vile katika joto la kiangazi.

5Kisha nilikujulisha dhambi yanguwala sikuficha uovu wangu.Nilisema, “Nitaungamamakosa yangu kwa Bwana.”Ndipo uliponisamehehatia ya dhambi yangu.

6Kwa hiyo kila mtu mcha Mungu akuombewakati unapopatikana,hakika maji makuu yatakapofurikahayatamfikia yeye.

7Wewe ndiwe mahali pangu pa kujificha,utaniepusha na taabu
na kunizunguka kwa nyimbo za wokovu.

8Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea;nitakushauri na kukuangalia.

9Usiwe kama farasi au nyumbuwasio na akili,ambao ni lazima waongozwe kwa lijamu na hatamula sivyo hawatakukaribia.

10Mtu mwovu ana taabu nyingi,bali upendo usio na kikomo wa Bwana
unamzunguka mtu anayemtumaini.

11Shangilieni katika Bwana na mfurahi, enyi wenye haki!Imbeni, nyote mlio wanyofu wa moyo!